
Samawati Safari
June 19, 2025 at 05:38 PM
*Karibu Arusha National Park – Luluti la Asili Karibu na Mji!*
Dakika chache tu kutoka Jiji la Arusha, Arusha National Park ni hazina iliyojificha yenye mandhari ya kuvutia, mlima wenye changamoto, na wanyama wa kipekee.
*Vivutio Unavyoweza Kufurahia:*
🌋 *Mlima Meru* – fursa ya kipekee ya kupanda mlima wa pili kwa urefu Tanzania
🦩 *Ziwa Momella* – lenye flamingo na mandhari ya kupendeza kwa picha
🦒 *Wanyama pori* – twiga, pundamilia, nyani wa colobus, na wengine wengi
🌿 *Ngurdoto Crater* – kasoko yenye mandhari ya kijani na wanyama
*Shughuli:*
- Kutembea msituni na askari
- Safari ya boti kwenye ziwa
- Kupiga picha za asili na ndege wa aina mbalimbali
- Kupanda Mlima Meru kwa wapenda adventure
*Tovuti rasmi:*
🌐 www.tanzaniaparks.go.tz
Arusha National Park ni mahali pa amani, uzuri na maajabu – mahali ambapo safari yako inaanza kwa ladha ya kipekee ya Tanzania!