Samawati Safari
Samawati Safari
June 19, 2025 at 08:53 PM
🥤Mwaka 2014 nilianza mipango ya ndoa, lakini kabla sijafanya uamuzi rasmi, nilipatwa na tatizo lingine. Mguu wa kushoto ukaanza kuvimba, na “mashine” ikaanza kushindwa kazi. Ilifika wakati hata kutembea ilikuwa shida. Nilipata msaada kutoka kwa rafiki yangu mmoja ambaye alijitolea kuniandamana hospitali mbalimbali kutafuta tiba. Nilitumia tiba mbadala kama kongoro, dagaa na bamia, pamoja na dawa za Kisunna—na hatimaye mashine ikarudi sawa. 🥤Nilitaka kuthibitisha kwamba nimepona kweli... ndipo nikajikuta nikipitia kipindi kigumu cha majaribio ya kingono. Nilitoka na wanawake wengi ndani ya muda mfupi tu—takriban 150! Ndiyo, 150. Nilitaka kuhakikisha mashine ipo imara. Baada ya hayo yote, nilihakikisha hali yangu ni nzuri na nikaendelea na mipango ya maisha. 🥤Mwaka 2016 nilijikuta napata fedha nyingi kupitia biashara ndogo ndogo na juhudi zangu binafsi. Nikaanza mipango ya kujitoa kwenye mikono ya wenye nyumba kwa kununua kiwanja changu. Siku moja jioni, mama mwenye nyumba alinikuta na kuniambia, “Nasikia umenunua kiwanja, hongera.” Nikashangaa! Nilikuwa sijamwambia mtu yeyote. Mipango yote ilikuwa ya siri sana. 🥤Nilikisia labda aliwahi kunisikia nikiongea na simu, au wapangaji wengine walimwambia. Nilishtuka lakini nikajipa moyo. Sikuweka maanani sana—nikaendelea na mipango ya ujenzi. Mwezi Julai mwaka huo, mke wangu alisafiri. Ndipo ndoto zile za kushiriki tendo la ndoa na mama mwenye nyumba zikaanza tena—lakini safari hii kwa nguvu na ukali zaidi. 🥤Kilichonisumbua ni kuwa, kila nikiamka, nilikuta ushahidi kuwa kilichotokea ndotoni ni kweli. Hali hii ikawa ya kila siku hadi nikaamua kuanza kumwangalia mama mwenye nyumba kwa makini kila asubuhi—lakini akawa hawezi kuniangalia usoni hata mara moja. Hapo nikaanza kupata hisia kuwa kuna kitu hakipo sawa
👍 1

Comments