
Samawati Safari
June 19, 2025 at 08:53 PM
🥤Siku moja nimerudi tu kutoka kazini, nikahisi mguu wa kulia una maumivu ya ghafla. Siku iliyofuata, hali ikazidi—nikashindwa hata kutoka nje kwenda kazini.
Nikaenda hospitali kufanya X-ray, lakini daktari alisema hanaona tatizo. Baada ya kumshinikiza, alifichua kuwa amegundua kitu kisicho cha kawaida ndani ya mguu wangu.
🥤Daktari aliniambia kuwa kuna sihiri (uchawi) kwenye mguu wangu. Kwa maneno mengine, kuna nguvu za giza ziko ndani yangu. Alinionya kuwa kesi kama hizo huwa hazitibiki hospitalini, bali kwa njia maalum.
Pamoja na wasiwasi, nilimkubalia na nikaanza safari ya tiba ya kiroho.
🥤Ndipo nikaanza kujifunua ukweli wa kushangaza na wa kutisha:
----Ile "ndoto" ya kushiriki tendo la ndoa na mama mwenye nyumba—haikuwa ndoto, bali ni kweli. Alikuwa anakuja chumbani kwangu usiku kupitia njia za kishirikina.
----- Alikuwa anachukua mbegu zangu kimwili na kuondoka nazo.
------ Hakupendezwa kabisa na mimi kununua kiwanja na kutoka kwenye nyumba yake.
🥤Baada ya kufanya uchunguzi zaidi, niligundua nyumba hiyo ya mama mwenye nyumba ilikuwa na historia ya ajabu. Wapangaji waliowahi kuishi hapo wengi wao hawakudumu—walikuwa wanahama ghafla bila kueleza mengi.
Kwa bahati nzuri, nilipata tiba, nikapona, na nilipohakikisha afya yangu imerejea vizuri, nilisubiri mke wangu arudi ndipo nikahama.
👍
1