Samawati Safari
Samawati Safari
June 19, 2025 at 08:54 PM
🥤Ninashukuru nilipona, lakini najua wapo wengi ambao bado wako kwenye nyumba hizo, wanalala na wachawi bila kujua, wananyang’anywa nyota zao bila kujitambua. Mwaka 2016 niliyaacha yote nyuma. Leo hii, nikiangalia nyuma, najua bila shaka: ilikuwa nyumba ya kishirikina. 🥤Ushuhuda huu nimeuandika kwa moyo wa kuwatahadharisha wapangaji wengine. Sio kila mwenye nyumba ana roho nzuri. Wengine hutumia wapangaji wao kama “chanzo cha nguvu” za kishirikina. Kumbuka: nyumba ni pahali pa mapumziko ya roho—ukiishi sehemu yenye nguvu mbaya, maisha yako yote huweza kwenda mrama. 🥤Niliamua kuweka baadhi ya vipande pembeni ili kupunguza urefu, lakini ukweli ni kwamba haya yote yalinitokea mimi binafsi. Na ninayaandika nikiwa mzima wa afya na akili timamu. Ukweli huu si wa kufurahisha—lakini ni wa muhimu. 🥤Wengine walipoisikia hii hadithi waliogopa sana. Lakini kuna muda hofu huokoa roho. Ushauri wa mwisho: Usipojua sababu ya mateso yako—jaribu kuangalia mahali unapoishi. Si kila mguu unaouma unatokana na kisukari, na si kila mashine inayokataa kazi ina hitilafu ya kawaida. 🥤Kuna nguvu nyingine ambazo haziwezi kutibiwa kwa Panadol wala X-ray. Wapo wataalamu wa kweli wa tiba mbadala. Ukiamini na kuchukua hatua, unaweza kupona. Kama mimi nilivyopona. Na leo hii nashukuru Mungu – nilihama, nikaishi kwa amani. 🥤Kama umefika hapa, share na wengine. Hii ni simulizi ya kweli – huenda ikamfungua macho mtu mwingine
👍 1

Comments