
Samawati Safari
June 20, 2025 at 09:06 PM
🥤Siku moja, mwanafunzi mmoja alikataa kula kabisa chakula cha shule. Alilia akisema:
“Chakula hiki kinanuka kama mtu aliyekufa.”
Tulidhani anatania, lakini kila siku aliendelea kugoma, hadi tukaanza kumpeleka nyumbani wakati wa chakula.
🥤Kilichotokea wiki moja baadaye kilibadilisha kila kitu.
Ijumaa moja jioni , tulikuwa kwenye kikao cha maandalizi ya mitihani. Watoto wachache wa bweni walikuwa wakicheza nyuma ya jiko ghafla Wakapiga kelele zilizotufanya tutoke ofisini mbio hadi nyuma ya jiko. Moja ya wanafunzi akasema
“Mkono! Mkono wa mtoto uko kwenye ndoo ya maji!”
🥤 Kabla hatujakaribia, anti zena alikuwa tayari ameshakimbilia pale, akaondoa ndoo na kuwambia wale watoto. Akasema:
“Huo ni mfupa wa kuku mlikula jana. Hamna mkono wowote.” Lakini macho ya mmoja wa walimu yalimwona akibeba kitu kwenye mfuko mweusi na kukificha ndani ya storeroom yake. Kwa kuwa hakuwa anaruhusu mtu kuingia humo, haikuwezekana kujua nini kilikuwemo.
🥤Jioni ile, mwalimu mwenzangu ambaye alikuwa na asili ya mkoa wa Tanga, alinishauri tuende kwa mtaalamu mmoja maarufu wa asili.
Tulifika kwake. Bila kupoteza muda, mzee huyo alitazama kwenye chungu chake, akasema:
🗣️ “Mpishi huyo si wa kawaida. Anatumia mkono huo kupika chakula kiive vizuri na kwa haraka pia kiwe kitamu ili wanafunzi wapendezwe na chakula chake aendelee kufanya kazi hapo shuleni. Anatumia mkono wa mtoto ".