Samawati Safari
Samawati Safari
June 20, 2025 at 09:07 PM
🥤Tulibaki hatujui la kusema. Mzee huyo aliongeza: “Kila anayekula chakula hicho analishwa ushawishi wa kichawi – ndio maana watoto wanapenda chakula kuliko hata familia zao." Siku iliyofuata, mtoto mmoja alianza kutapika damu baada ya uji wa asubuhi. Tukatoa taarifa kwa uongozi wa shule na serikali ya mtaa. Lakini hakuna aliyeamini. Mkuu wa shule alisema kama ni kweli kwann matukio kama haya yasingekuwepo toka zamani, huyu n mpishi wetu wa muda sana acheni kutuaminisha mambo ya ajabu, yeye kama anatumia kwa nia njema na chakula chake hakina madhara kwa watoto Mwacheni, kwanza hayo mambo ni imani potofu, huyu n mpishi wetu na ataendelea kuwa mpishi wetu milele, siwezi kumfukuza kazi". Mku wa shule aliondoka na kutuacha tumesimama pale nje ya ofisi yake. Nilijiona kama mtu wa ajabu sana. Mwaka uliofuata nilipata kazi sehemu nyingine na kuhama pale shuleni. 🥤 Yule jamaa yangu niliyemuacha pale alisema kuwa yule mpishi aliacha kazi baada ya miaka miwili mbele. Saizi ile shule inampishi mwingine ila wanafunzi wanalalamika sana chakula kibichi muda mwingine maharage hayana chumvi kabisa. Uongozi wa shule umejaribu kutafuta mpishi mwingine kila wanaemwambia anakataa kufanya kazi kwenye ile shule sababu mshahala ni mdogo sana

Comments