
TBS - Viwango
June 19, 2025 at 06:04 AM
Mkurugenzi Mkuu (TBS) Dkt. Ashura Katunzi, akitoa taarifa ya mafanikio TBS iliyoyapata kupitia mradi wa QUALITAN wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya maabara chini ya ufadhili wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya ( EU), mapema leo jijini Dar es salaam.
Dkt. Katunzi amesema mradi huu mbali na kusaidia ununuzi wa vifaa pia umeweza kuijengea uwezo taasisi katika masuala ya kidijitali, miundo mbinu ya mifumio na mafunzo ya kitaalam.
