THE ISLAMIC FOUNDATION
THE ISLAMIC FOUNDATION
June 20, 2025 at 11:33 AM
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu elimu hapa nchini pamoja na kutatua changamoto mbalimbali kwa wanafunzi ikiwemo suala zima la mikopo ili waweze kugharamikia mahitaji yote muhimu wakiwa vyuoni. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni Rasmi akimwakilisha Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu cha Waislmu cha Morogoro (MUM) Aidha Majaliwa ametoa ahadi ya kuchangia milioni 10 huku Mh. Rais Daktari Samia Suluhu Hassan naye akitoa ahadi ya mchango wa shilingi milioni 100 katika uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho.
Image from THE ISLAMIC FOUNDATION : WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema...
❤️ 1

Comments