IMANI MAWAIDHA CHANNEL
IMANI MAWAIDHA CHANNEL
June 9, 2025 at 06:29 AM
Haifai kufunga masiku haya ya Tashriyq hata kama mtu alikuwa na mazowea ya Swawm za Sunnah kama vile Jumatatu, Alkhamiys au Ayyaamul-Biydhw. Dalili ya makatazo ni katika Hadiyth ifuatayo: عن أبي هريرة أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ حُذَافَةَ يَطُوفُ فِي مِنًى أَنْ: ((لَا تَصُومُوا هَذِهِ الْأَيَّامَ فَإِنَّهَا أَيَّامُ أَكْلٍ وَشُرْبٍ وَذِكْرِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ)) Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma 'Abdullaah bin Hudhaafah azunguke Minaa na atangaze: "Msifunge siku hizi, kwani hizi ni siku za kula na kunywa na kumdhukuru Allaah ‘Azza wa Jalla.” [At-Twabariy 4: 211]
❤️ 👍 2

Comments