IMANI MAWAIDHA CHANNEL
IMANI MAWAIDHA CHANNEL
June 12, 2025 at 07:05 PM
*TUNAKUMBUSHANA KWENYE KHAYRAT MIRADI IJUMAA* Tunawaomba ndugu zetu wapendwa, kesho inshaAllah pindi Allah atakapokujaalia uhai na afya ukaamka salama, tafadhali changia kwa kununua Juzuu – iwe ni moja, mbili, au hata zaidi – kadri uwezo wako unavyoruhusu. Lengo letu ni kukusanya Juzuu 2,000 zitakazosaidia madarasa ya Qur’an katika maeneo ya mashinani na mikoani ambako kuna uhaba mkubwa wa vitabu hivi vitukufu. Walimu wengi wana moyo wa kufundisha na hamu kubwa ya kuwaendeleza watoto katika elimu ya Qur’an, lakini hukwama kutokana na changamoto za vifaa, hususan upungufu wa Juzuu. Kwa mchango wako, utakuwa sehemu ya kueneza elimu ya dini na kuwainua watoto wetu katika njia ya haki na nuru. Kila herufi itakayosomewa kutokana na Juzuu uliyochangia, thawabu yake itarudi kwako bila kupungukiwa. Mchango wako leo, ni sadaka yenye kuendelea milele.

Comments