IMANI MAWAIDHA CHANNEL
IMANI MAWAIDHA CHANNEL
June 20, 2025 at 03:19 AM
*Assalam alaykum warahmatuAllah wabarakat.* *Baadhi ya mapambano hayaonekani.* Hakuna anayeyaona mawazo yanayokuzonga usiku wa manane, machozi unayoyamwaga kwa siri, au jitihada zako za kila siku kujituliza na kuendelea kusonga mbele. Lakini Allah anajua. Anaona uzito wa mzigo unaoubeba kimya kimya. Anayahesabu kila dua usiyoitamka kwa sauti, kila wakati unapoamua kuwa na subira ilhali ungeweza kujisalimisha. Uvumilivu huo wa kimya? Hauendi bure. Umeandikwa, unashuhudiwa, na utalipwa na Yule anayekufahamu kwa undani wa moyo wako – hata pale ambapo hakuna mwingine anayekuelewa.

Comments