
Bet Sure Tanzania
June 19, 2025 at 12:37 PM
SURA YA 4
Sauti ya Ndani — Mwandani au Adui?
Ndani ya kila binadamu kuna sauti ya siri. Sauti hii hunena kwa kimya, lakini huamua mengi katika maisha yetu.
Ni sauti tunayosikia kila tunapojaribu kujikubali, kujithamini, au kuchukua hatua mpya.
Lakini swali kuu ni:
Je, sauti yako ya ndani ni rafiki au ni adui?
Mkosaji wa Ndani (The Inner Critic)
Hii ni sauti inayokosoa, kukatisha tamaa, na kudharau kila jambo jema unalojaribu kufanya.
Sauti hii ilianza kuumbika tangu utoto — mara nyingi kutokana na:
Kukosolewa sana
Kutokukubalika
Kunyimwa uthibitisho ("affirmation")
Kushushwa thamani na wale uliowaamini
Wewe si mzuri vya kutosha
“Ukijaribu utashindwa tu.”
“Kuna wengine bora kuliko wewe
“Hutapendwa ukiwa hivi.”
Mwishowe, sauti hizo zikawa sehemu yako ya ndani kabisa — zikawa sauti yako mwenyewe.
Athari za Kuishi na Adui wa Ndani
Mkosaji wa ndani anakuambia:
Usianze biashara hiyo — si yako.
Usivae nguo hiyo — unachekesha.
Usijieleze — watakudharau.
Usiseme unachohisi — hutaheshimiwa.
Matokeo yake?
Unaishi maisha ya woga, aibu, kujificha na kujikana. Unaweka “mask” ili upendwe, huku moyoni ukihisi hutoshi.
Ukweli ni Huu: Sauti Hiyo Siyo Wewe
Sauti hiyo ya ukosoaji si wewe wa kweli.
Ni mchanganyiko wa maneno ya wazazi, walimu, jamii, na watu waliokuumiza.
Ili kupona na kujijenga, ni lazima uanze kuisikia, kuhoji na kuivunja.
Kuibadilisha Sauti ya Ndani
Hatua ya kwanza ya kuibadilisha sauti ya ndani ni kuitambua.
Jua wakati inapoongea, andika unachojisikia. Kisha jiulize:
Hii sauti inanisaidia au inaniharibu?
Ni nani alinifundisha kuzungumza hivi na nafsi yangu?
Ningemwambia hivi rafiki yangu? Kama sivyo, kwa nini nijiseme hivi mwenyewe
*🫳Badala ya kusema: “Mimi ni mzigo*
Sema: “Ninajifunza kubeba maisha yangu kwa upendo
Badala ya kusema: “Mimi ni mpumbavu
Sema: “Nimekosea, lakini bado najifunza — na ninatosha.”
Zoezi la Sura ya 4 — Kukabiliana na Mkosaji wa Ndani
tafakali kwa.dk 3/5 halafu ujipe majibu mwenyewe
1. Ni kauli gani ya ukosoaji unajikuta ukiisema mara kwa mara moyoni mwako?
2. Ni nani wa kwanza aliyekufundisha kujiona kwa njia hiyo?
3. Ni uongo gani mkosaji wa ndani amekuambia hadi leo?
4. Sasa, andika jibu la kweli kwa kila uongo huo kwa sauti ya upendo.
5. Tunga maneno ya uthibitisho (affirmation) yako mwenyewe, mfano:
"Ninatosha vile nilivyo
"Nastahili upendo na mafanikio
"Sauti yangu ina thamani
Hitimisho la Sura
Kila wakati unavyoamua kuzungumza kwa upendo na nafsi yako, unamnyamazisha mkosaji wa ndani, na kumkaribisha rafiki mpya — sauti yako ya kweli, iliyojaa huruma, ujasiri na matumaini.
Wakati mwingine adui yako mkubwa zaidi anakaa kichwani mwako. Lakini kwa upendo, anaweza kuwa rafiki yako wa karibu
👍
1