BashBuzz
BashBuzz
June 19, 2025 at 08:34 AM
*TAHADHARI YA UPEPO MKALI KILIFI* Idara ya utabiri wa hali ya hewa kaunti ya Kilifi imetoa tahadhari kwa wakaazi wa kaunti hio kuwa makini kwani kuanzia leo Alhamisi hadi Jumamosi kunatarajiwa upepo mkali ambao huenda ukasababisha uharibifu. Idara hio imeongeza kuwa upepo huo utapungua siku ya Jumapili lakini unatarajiwa utaongezeka tena Jumatatu juma lijalo hivyo idara hio imewatahadharisha wavuvi dhidi ya kutumia maboti madogo kwenye maji makuu ya bahari hindi. Pia katika kipindi hicho kutakua na mvua za hapa na pale katika kaunti ya Kilifi. 📹 | Khalil

Comments