BashBuzz
BashBuzz
June 20, 2025 at 07:07 PM
*Gavana Mung’aro Afarijiwa na Viongozi wa Dini kutoka Malindi* Viongozi wa dini ya Kiislamu kutoka Malindi wamemtembelea Gavana wa Kaunti ya Kilifi, Mheshimiwa Gideon Mung’aro, ili kumfariji na kumpa pole kufuatia kifo cha baba yake mzazi, Mzee Baya Mung’aro Senior. Ujumbe huo uliongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Malindi na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Kiswahili, Mheshimiwa Abubakar Badawy, aliyekuwa kansela katika wadi ya shella, Muheshimiwa Ahmed Abdulrahman 'Bahry', Kansela wa zamani Mh. Ali Sheemaka, pamoja na mwanaharakati wa kupambana na matumizi ya mihadarati katika Kaunti ya Kilifi, Sheikh Famau Mohamed Famau miongoni wa viongozi wengine.
Image from BashBuzz: *Gavana Mung’aro Afarijiwa na Viongozi wa Dini kutoka Malindi*   Viong...

Comments