Samawati Safari
Samawati Safari
June 21, 2025 at 08:15 AM
Katika miaka ya hivi karibuni, dunia imeendelea kushuhudia machafuko, maandamano, mauaji ya raia, mashambulizi ya angani, na vikwazo vinavyoathiri maisha ya watu wa kawaida, hususan watoto na wanawake. Makubaliano mengi ya amani yamekuwepo kwenye karatasi lakini hayajatekelezwa kikamilifu kutokana na kutokuaminiana baina ya pande mbili, na uingiliaji wa mataifa mengine yenye maslahi tofauti. Mgogoro huu umekuwa wa muda mrefu kuliko wengi ulimwenguni, ukihusisha masuala ya haki ya ardhi, utaifa, dini, na kumbukumbu za kihistoria. Wakati baadhi ya mataifa yanaanza kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel, bado suala la Palestina limeendelea kusalia kama jeraha linalohitaji tiba ya haki, si tu kwa ajili ya siasa bali kwa utu wa binadamu. Dunia inaendelea kutafuta njia ya kuleta suluhisho la kweli, lakini mpaka sasa, bado damu inamwagika, na ndoto ya amani ya pamoja inasalia kuwa mbali na utekelezaji. Kwa Leo Ngoja niishie HAPA.
❤️ 🍎 2

Comments