Samawati Safari
Samawati Safari
June 21, 2025 at 08:41 PM
Yule kijana hakusema kitu aliingia ndani, akiwa n mwenye woga na hofu kubwa sana, alienda hadi kitandani na kulala. Kesho yake, walikula nyama tena. Bibi yake alisema, “Leo ni nyama tamu  imetoka mbali sana.” Samwel alilia kwa uchungu sana. Alianza kupata ndoto za ajabu  wanawake wakiwa uchi, wakimlilia na kusema, “Tusemeeni…” 🥤Siku moja, alienda kwao na rafiki yake  mmoja wa pale  kijijini, alipofika aliwakuta rafiki yake ameketi na Babu yake wakipga story. Yule Babu alipomuona Samuel alishtuka na kusema aliyesemekana alikuwa na macho ya rohoni “Umejaa damu ya watu ndani ya tumbo lako. Ondoka nyumbani hapo mara moja.”
🍎 👍 2

Comments