Samawati Safari
Samawati Safari
June 21, 2025 at 08:42 PM
🥤Yule kijana alioogopa sana alitoroka usiku wa saa tisa, akakimbilia kituo cha polisi cha Tukuyu. Aliwaambia kila kitu. Aliwapeleka Polisi kijijini kwao kesho yake, lakini walikuta nyumba ikiwa wazi, bila mtu. Bibi Nshubali alitoweka hakuwepo kwenye ile nyumba. 🥤Uchunguzi ulipoanza, walikuta mifupa iliyofukiwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao. Kijiji kilipatwa na taharuki. Wazee walikumbuka kwamba bibi huyo aliletwa kijijini miaka mingi nyuma na hakuwahi kuolewa. Alikuwa peke yake, lakini kila wakati alikuwa na chakula kingi na pesa zisizoeleweka. 🥤Yule kijana alipelekwa kwenye kituo cha watoto yatima mjini Mbeya. Alikaa kimya kwa miaka mingi, Miaka ya  baadaye, akiwa mtu mzima, alianza kuota  ndoto zinazojirudia. Alikuwa anaota akikatakata nyama, kwa pembeni kulikuwa watoto wakimwangalia wakiwa na huzuni sana. 🥤Alianza safari ya ndani – alitembelea makaburi ya kijiji chao, alijitolea kusaidia familia zilizopoteza wapendwa wao, na akaanza kuandika historia ya maisha yake. 🥤Aliamua kuandika kitabu chake kinachoitwa “Nyama ya Siri”. Alisema, “Sikuchagua kulelewa maisha ya kichawi, hajawahi kurudi kuishi kule kijijini kwao , lakini kila mwaka hutuma sadaka kwa kanisa la kijiji na kile kituo cha watoto yatima 🥤Hadithi ya kijana huyu inabaki kama onyo. Si kila bibi ni mpenzi wa wajukuu. Wengine ni wachawi na walaji wa nyama na damu za watu
👍 🍎 3

Comments