DEFO - TANZANIA WhatsApp Channel

DEFO - TANZANIA

82 subscribers

About DEFO - TANZANIA

Jifunze na fahamu ujuzi, teknolojia, vipaji na masuala mbalimbali ya watu wenye mahitaji maalumu wa Tanzania.

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

DEFO - TANZANIA
DEFO - TANZANIA
1/31/2025, 3:55:08 PM

Ulemavu wa *uziwi* ni hali ambapo mtu anapata shida au kupoteza kabisa uwezo wa kusikia. Hii inaweza kuwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kiafya, majeraha, au hali za kimaumbile. Ulemavu wa kiziwi unaweza kuwa wa kudumu au wa muda, na unaweza kutokea kwa njia nyingi tofauti. Hapa chini, tutaangazia baadhi ya sababu kuu za mtu kuwa mlemavu wa uziwi. *Sababu za Mtu Kuwa Mlemavu wa Uziwi:* 1. *Magonjwa ya Masikio:* Magonjwa kama maambukizi ya masikio (otitis media), masikio ya maji, au magonjwa mengine ya masikio yanaweza kusababisha kupoteza uwezo wa kusikia. Ikiwa magonjwa haya hayatapatiwa tiba mapema, yanaweza kuwa sababu ya ulemavu wa kudumu wa kusikia. 2. *Maumbile ya Kuzaliwa:* Baadhi ya watu huzaliwa wakiwa na ulemavu wa uziwi kutokana na sababu za maumbile. Hii inaweza kuwa ni kutokana na matatizo ya jeni au hali ya kiafya ya mama wakati wa ujauzito, kama vile, maambukizi ya rubella au homa ya mapafu. Inaendelea.......................

Image
DEFO - TANZANIA
DEFO - TANZANIA
1/31/2025, 4:02:12 PM

*3. Kuzeeka (Umri Mkubwa):* Kadri mtu anavyozeeka, uwezo wake wa kusikia unaweza kupungua kwa asili. Hali hii inajulikana kama presbycusis, na hutokea kutokana na mabadiliko ya kiasili katika masikio na njia za usikivu. *4. Maumivu au Jeraha la Kimwili:* Maumivu au jeraha kwenye masikio, kichwa, au shingo yanaweza kuathiri vibaya uwezo wa kusikia. Hii inaweza kutokea kutokana na ajali, kuanguka, au majeraha mengine kama kumwagikiwa na tindikali. 5. *Matumizi ya Sauti Kali kwa Muda Mrefu:* Kusikiliza sauti kali sana, kama vile kwenye tamasha la muziki au kutumia headphones kusikiliza mziki kwa sauti kubwa kwa muda mrefu, kunaweza kusababisha uharibifu wa seli za masikio na hivyo kusababisha kupoteza uwezo wa kusikia. *6. Matatizo ya Damu au Shinikizo la Damu:* Magonjwa yanayohusiana na shinikizo la juu la damu (hypertension) au matatizo ya mzunguko wa damu yanaweza kuathiri usikivu wa mtu. Hii inaweza kuathiri neva za kusikia au kupunguza mtiririko wa damu kwa masikio. *7. Matatizo ya Neva au Ubongo:* Wakati mwingine matatizo ya neva au ubongo kama vile multiple sclerosis au stroke yanaweza kuathiri uwezo wa kusikia. Hii inapotokea, mtu anaweza kuwa na ulemavu wa kusikia licha ya kuwa na masikio yenye afya.

DEFO - TANZANIA
DEFO - TANZANIA
1/31/2025, 4:06:02 PM

*8. Madhara ya Dawa:* Baadhi ya dawa za tiba, hasa zile zinazotumika kwa ajili ya magonjwa ya saratani, HIV/AIDS, au magonjwa ya moyo, zinaweza kuwa na madhara kwa masikio na kusababisha upotevu wa kusikia. *9. Ugonjwa wa Moyo au Kifua:* Magonjwa ya moyo na kifua yanaweza kuathiri usikivu wa mtu ikiwa yanahusiana na kupungua kwa oksijeni au mzunguko wa damu unaohitaji kuendesha mifumo ya kusikia. *10. Maambukizi ya Virusi:* Maambukizi ya virusi kama measles (rubella), mumps na meningitis yanaweza kusababisha ulemavu wa kudumu wa kusikia. Hii ni hasa ikiwa maambukizi haya yanapoharibu maeneo muhimu ya masikio ya ndani au neva za kusikia. Imeandaliwa na; Hamza Masudi Ngosse 👂👂🦻👂🦻

👍 1
DEFO - TANZANIA
DEFO - TANZANIA
2/2/2025, 8:08:31 PM

https://docs.google.com/forms/d/10sypNwTXp1wT7vMPOAgF_p4z0AJ9tnc8JQDyh0rMilE/edit

DEFO - TANZANIA
DEFO - TANZANIA
2/4/2025, 9:44:59 PM

TUMEBAKIZA SIKU 3 PEKEE🥳🥳 TWENZETU CHARITY #elimikanawalemavu #disability #hajimanara #jongeanamlemavu https://www.instagram.com/reel/DFqpReBtMnl/?igsh=MWpsYnNlZXBxMjdyOA==

DEFO - TANZANIA
DEFO - TANZANIA
2/6/2025, 8:17:08 AM

*Taarifa kwa umma* Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu iliyopo Arusha imetoa uamuzi katika kesi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na mashirika mengine ya kimataifa waliofungua kesi dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mashirika matatu ndiyo waombaji katika kesi hii na wanadai ukiukwaji wa haki kadhaa za watu wenye ualbino. UTSS Canada ilishiriki kama AMICUS (rafiki wa mahakama katika kusaidia kutoa maamuzi) Hukumu imetolewa Feb 5 2025 jijini Arusha na mahakama hiyo. Haya ni kwa muhtasari maagizo ambayo yametolewa na mahakama hiyo:- ✅⁠ ⁠ Serikali kuanzisha kwa mfuko wa fidia kwa walioathirika na madhila. ✅ ⁠ Serikali kurekebisha sheria zilizopo ili kuainisha na kuadhibu vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino. ✅ Serikali kubuni na kutekeleza mikakati ya haki na ustawi wa watoto wenye ualbino, ikiwa ni pamoja na usalama wao, msaada wa kisaikolojia, matibabu. ✅ Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ya Uchawi ya mwaka 1928, Sura ya 18 ya Sheria za Tanzania, ili kuondoa utata uliopo kuhusu uchawi na tiba za asili. ✅ Serikali kuchukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha upatikanaji wa haki ya elimu, huduma za afya ✅ Serikali kuhamasisha jamii kuhusu imani potofu zinazohusiana na ualbino kwa kufanya kampeni za kina zitakazoendelea kwa muda wa angalau miaka miwili ✅ Serikali iliagizwa kuchapisha uamuzi wa Mahakama ndani ya miezi mitatu tangu tarehe ya kupokea taarifa hiyo. ✅ Serikali iliagizwa kuwasilisha ripoti kuhusu hali ya utekelezaji wa maamuzi hayo ndani ya kipindi cha miaka miwili. ✅ Serikali ilielezwa endapo uamuzi huo hautakuwa umetimizwa kikamilifu ndani ya miaka mitatu tangu ilipotolewa taarifa, Mahakama itafanya kikao cha ufuatiliaji wa utekelezaji. *Imetolewa na UTSS Canada* *6 Feb 2025*

DEFO - TANZANIA
DEFO - TANZANIA
2/9/2025, 8:22:30 PM

HODIII HODIIII Kesho kuanzia Saa mbili Asubuhi @defotanzania🇹🇿 tumealikwa kwenye kipindi katika Station ya Taifa ambayo ni TBC, na Raisi Mama Dr. Samia Suluhu Hassan🇹🇿 na Watumishi wote watatusikiliza Macomrade (Vijana wao). Kuingumzia taasisi yetu na kwenda kuuhabarisha umma juu ya Utetezi na Uenezaji wa uelewa juu ya Haki za Watu wenye Ulemavu Nchini Tanzania.🇹🇿

☺️ 1
DEFO - TANZANIA
DEFO - TANZANIA
2/20/2025, 6:52:10 PM

It's amazing and good news to us🛝

👍 1
Video
Link copied to clipboard!