
DEFO - TANZANIA
February 6, 2025 at 08:17 AM
*Taarifa kwa umma*
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu iliyopo Arusha imetoa uamuzi katika kesi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na mashirika mengine ya kimataifa waliofungua kesi dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mashirika matatu ndiyo waombaji katika kesi hii na wanadai ukiukwaji wa haki kadhaa za watu wenye ualbino. UTSS Canada ilishiriki kama AMICUS (rafiki wa mahakama katika kusaidia kutoa maamuzi)
Hukumu imetolewa Feb 5 2025 jijini Arusha na mahakama hiyo.
Haya ni kwa muhtasari maagizo ambayo yametolewa na mahakama hiyo:-
✅ Serikali kuanzisha kwa mfuko wa fidia kwa walioathirika na madhila.
✅ Serikali kurekebisha sheria zilizopo ili kuainisha na kuadhibu vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino.
✅ Serikali kubuni na kutekeleza mikakati ya haki na ustawi wa watoto wenye ualbino, ikiwa ni pamoja na usalama wao, msaada wa kisaikolojia, matibabu.
✅ Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ya Uchawi ya mwaka 1928, Sura ya 18 ya Sheria za Tanzania, ili kuondoa utata uliopo kuhusu uchawi na tiba za asili.
✅ Serikali kuchukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha upatikanaji wa haki ya elimu, huduma za afya
✅ Serikali kuhamasisha jamii kuhusu imani potofu zinazohusiana na ualbino kwa kufanya kampeni za kina zitakazoendelea kwa muda wa angalau miaka miwili
✅ Serikali iliagizwa kuchapisha uamuzi wa Mahakama ndani ya miezi mitatu tangu tarehe ya kupokea taarifa hiyo.
✅ Serikali iliagizwa kuwasilisha ripoti kuhusu hali ya utekelezaji wa maamuzi hayo ndani ya kipindi cha miaka miwili.
✅ Serikali ilielezwa endapo uamuzi huo hautakuwa umetimizwa kikamilifu ndani ya miaka mitatu tangu ilipotolewa taarifa, Mahakama itafanya kikao cha ufuatiliaji wa utekelezaji.
*Imetolewa na UTSS Canada*
*6 Feb 2025*