
NENO LA LEO
36 subscribers
About NENO LA LEO
Pata Neno la Mungu kila siku likusaidie kwenye safari yako ya maisha
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Waebrania 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.


Isaya 48:17 SUV BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.


*MUNGU ANAJUA UNACHOKIFANYA* *(TUBIA DHAMBI ZAKO ZA SIRI)* *"Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?" β Isaya 29:15 (SUV)* Watu wengi wanaishi kana kwamba Mungu haoni. Lakini Isaya 29:15 ni onyo kwa wote wanaojaribu kuficha dhambi zao na kujifanya watakatifu mbele za watu. Mungu si kipofu. Anajua kila kitu (Omniscient), ana uwezo wote (Omnipotent), na yupo kila mahali (Omnipresent). Huwezi kukimbia macho Yake. Unachokifanya gizani, Mungu anakiona kama vile ni mchana mweupe. Hakuna mtu anayetaka kuonekana mwovu. Hakuna mtu anayetaka kuaibika hadharani. Lakini kwa bahati mbaya, kuna unafiki mwingi sana kanisani leo. Watu wanafanya machukizo kwa siri lakini wanajionyesha kuwa watakatifu, wapole, na wenye upendo mbele za watu. Wengine huenda mbali zaidi na kuwahukumu wengine kwa makosa madogo huku wao wakificha uovu mkubwa wanaoufanya kwa siri kwenye maisha yao. Mungu anasema: *βOle wenu.β* Kama unadhani Haoni kiburi chako, tamaa zako, uongo wako, udanganyifu wako, na dhambi zako za siriβamka! Acha kujificha. Acha kujifanya mtakatifu wakati moyo wako umejaa uchafu. Acha kujikuza wakati dhambi inatawala nafsi yako. Jinyenyekeze. Kama huwezi kuacha dhambi, mwombe Mungu akusaidie. Hauwezi kuishinda dhambi mwenyewe, wala usifiche hatia yako kwa kujiona mwenye haki. Toka gizani kabla Mungu hajakufichua. Maana akikuumbua, aibu yako itakuwa kubwa na haitakuwa tu hapa duniani bali hukumu ya milele inakusubiri motoni. Ujumbe huu si kwa mtu mwingine. Ni kwa ajili yako. Mungu anazungumza na moyo wako sasa hivi. Tubu. Kiri dhambi zako. Rudi kwa Mungu. Yuko tayari kukusamehe. Lakini usichelewe. Huna uhakika wa kesho kama utakuwepo. *Sala:* Bwana Yesu, unayajua maisha yangu. Nisaidie kuacha maovu yote. Nisamehe, nitakase, nibadilishe, na unipe maisha mapya. -β----------------------- Mwandishi: Mtumishi Lucas Kaaya Whatsapp Channel: https://whatsapp.com/channel/0029ValJYhIKQuJRtxwpDu1d


Zab 91:10 SUV Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.


Mithali 5:23 Atakufa kwa kukosa maonyo; Na kwa wingi wa upumbavu wake atapotea.


Isa 49:8 SUV BWANA asema hivi, Wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa.


Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, Ebr 12:1 SUV


Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Wagalatia 5:24 SUV


Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. Yohana 5:25 SUV
