NENO LA LEO
NENO LA LEO
June 17, 2025 at 05:44 AM
*MUNGU ANAJUA UNACHOKIFANYA* *(TUBIA DHAMBI ZAKO ZA SIRI)* *"Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?" — Isaya 29:15 (SUV)* Watu wengi wanaishi kana kwamba Mungu haoni. Lakini Isaya 29:15 ni onyo kwa wote wanaojaribu kuficha dhambi zao na kujifanya watakatifu mbele za watu. Mungu si kipofu. Anajua kila kitu (Omniscient), ana uwezo wote (Omnipotent), na yupo kila mahali (Omnipresent). Huwezi kukimbia macho Yake. Unachokifanya gizani, Mungu anakiona kama vile ni mchana mweupe. Hakuna mtu anayetaka kuonekana mwovu. Hakuna mtu anayetaka kuaibika hadharani. Lakini kwa bahati mbaya, kuna unafiki mwingi sana kanisani leo. Watu wanafanya machukizo kwa siri lakini wanajionyesha kuwa watakatifu, wapole, na wenye upendo mbele za watu. Wengine huenda mbali zaidi na kuwahukumu wengine kwa makosa madogo huku wao wakificha uovu mkubwa wanaoufanya kwa siri kwenye maisha yao. Mungu anasema: *“Ole wenu.”* Kama unadhani Haoni kiburi chako, tamaa zako, uongo wako, udanganyifu wako, na dhambi zako za siri—amka! Acha kujificha. Acha kujifanya mtakatifu wakati moyo wako umejaa uchafu. Acha kujikuza wakati dhambi inatawala nafsi yako. Jinyenyekeze. Kama huwezi kuacha dhambi, mwombe Mungu akusaidie. Hauwezi kuishinda dhambi mwenyewe, wala usifiche hatia yako kwa kujiona mwenye haki. Toka gizani kabla Mungu hajakufichua. Maana akikuumbua, aibu yako itakuwa kubwa na haitakuwa tu hapa duniani bali hukumu ya milele inakusubiri motoni. Ujumbe huu si kwa mtu mwingine. Ni kwa ajili yako. Mungu anazungumza na moyo wako sasa hivi. Tubu. Kiri dhambi zako. Rudi kwa Mungu. Yuko tayari kukusamehe. Lakini usichelewe. Huna uhakika wa kesho kama utakuwepo. *Sala:* Bwana Yesu, unayajua maisha yangu. Nisaidie kuacha maovu yote. Nisamehe, nitakase, nibadilishe, na unipe maisha mapya. -‐----------------------- Mwandishi: Mtumishi Lucas Kaaya Whatsapp Channel: https://whatsapp.com/channel/0029ValJYhIKQuJRtxwpDu1d
Image from NENO LA LEO: *MUNGU ANAJUA UNACHOKIFANYA* *(TUBIA DHAMBI ZAKO ZA SIRI)*  *"Ole wao ...

Comments