Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #fleetexpansion
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "As Salaam Air yaongeza ndege ya nne aina ya Embraer 120. Shirika la ndege la @assalaamairtz , lenye makao makuu visiwani Zanzibar, hivi karibuni limepokea ndege nyingine aina Embraer 120 yenye namba ya usajili 5H-LUF. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao wa Plane Spotter, ndege hiyo yenye iliwasili kwa mara ya kwanza katika Kisiwa cha Pemba juni 4 2025, ikitokea Zanzibar (ZNZ) na kutua salama katika Uwanja wa Ndege wa Pemba (PMA) majira ya saa 11:38 jioni Safari iliyochukua dakika 22 pekee. As Salaam ilianzishwa rasmi mwaka 2011 likifanya safari za Arusha-Zanzibar, Dar es Salaam-Pemba, Dar es Salaam-Zanzibar, Pemba-Dar es Salaam,Pemba-Zanzibar, Zanzibar-Arusha na Zanzibar-Pemba. Kwa sasa kampuni hiyo ina jumla ya ndege nne aina ya Embraer 120, kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 30. . #airline #assalaamair #fleetexpansion #newaircraft #assalaamair #embraer120 #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"
https://www.instagram.com/reel/DKrjPckNXRJ/?igsh=MWU4M2x4Nm0zMTNqcg== *As Salaam Air yaongeza ndege...
Aviation Tanzania on Instagram: "Delta Airlines yaielekeza ndege yake mpya Tokyo kukwepa ushuru wa Marekani. Kampuni ya ndege ya Delta Airlines imepokea ndege mpya aina ya Airbus A330-900neo yenye namba ya usajili N435DX. Ndege hiyo iliondoka kutoka Toulouse-Blagnac (TLS) nchini Ufaransa Mei 30 na kutua Tokyo Narita (NRT) nchini Japan baada ya safari ya zaidi ya masaa 16. Badala ya kupelekwa Marekani kama kawaida, ndege hiyo ilielekezwa Tokyo ili kukwepa ushuru wa Marekani unaotozwa kwa ndege mpya zinazoingizwa moja kwa moja nchini humo. Shirika hilo limechukua hatua hii kama mbinu mbadala ya kuendelea kuongeza ndege mpya bila kugharamika zaidi kutokana na ushuru wa Marekani. #ustariffs #airlines #deltaairlines #fleetexpansion #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DKZEjFEMhmH/?igsh=ZWMxY3Rja2NibnNs *Delta Airlines yaielekeza ndege yak...
Aviation Tanzania on Instagram: "Qatar Airways yatupilia mbali agizo la ndege 25 za Boeing 737 MAX 10. Shirika la ndege la Qatar Airways limethibitisha kusitisha mpango wake wa kununua ndege 25 aina ya Boeing 737 MAX 10, uamuzi ambao unatamatisha rasmi agizo hilo lililotolewa mwaka 2022 katika Maonyesho ya Anga ya Farnborough. Katika mahojiano na chombo cha habari cha Bloomberg, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Badr Al-Meer, alifichua hatua hiyo, akiielezea kuwa ni sehemu ya mabadiliko ya mikakati ya shirika hilo katika usafiri wa ndani na wa masafa mafupi. Uamuzi huu umekuja wakati Qatar Airways ikiwa tayari imesaini agizo jipya la ndege zenye thamani ya dola bilioni 96 za Kimarekani kwa ndege 160 aina ya Boeing 787 na 777X, lakini imeamua kuachana kabisa na ndege za Boeing MAX 10. Mpango wa kufuta agizo hilo ulianza kuvuma Disemba mwaka jana, huku vyanzo vya habari vikidokeza kuwa MAX 10 haikidhi tena mahitaji ya sasa ya mtandao wa ndege za Qatar Airways. Ilitarajiwa kuwa shirika hilo huenda lingebadilisha agizo hilo na kuagiza Boeing 737 MAX 8, lakini hatimaye likachagua kufuta agizo lote. Agizo hilo lilitangazwa kwenye maonyesho ya Farnborough mwaka 2022 na aliyekuwa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Boeing Commercial Airplanes, Stan Deal, ambaye aliitaja MAX 10 kama chaguo bora kwa mtandao wa safari za kikanda za Qatar Airways. Kwa sasa, Qatar Airways inaelekeza mikakati yake katika safari za masafa mafupi kwa kuagiza ndege kutoka kampuni ya Airbus. Kwa mujibu wa takwimu za ch-aviation, shirika hilo lina ndege 50 aina ya Airbus A321neo ambazo bado hazijakabidhiwa. #fleetexpansion #airline #qatarairways #boeing737max10 #airbus #farnboroughinternationalairshow #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DKHgrO4MvtT/?igsh=MXRmdHg1bnJlNWNnOQ== *Qatar Airways yatupilia mbali a...
Aviation Tanzania on Instagram: "Ethiopian Airlines yapokea ndege mpya ya Boeing 777-200LR, ya mwisho kutengenezwa na Boeing. Shirika la Ndege la @fly.ethiopian kupitia kitengo chake cha mizigo, Ethiopian Cargo, limepokea ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 777-200LR Freighter yenye namba ya usajili ET-BAC. Kupokelewa kwa ndege hii ni tukio la kihistoria kwani ndio ndege ya mwisho ya aina hii kutengenezwa na kampuni ya Boeing, hivyo Boeing imekamilisha uzalishaji wa mojawapo ya ndege bora na zenye uwezo mkubwa katika historia ya usafirishaji wa mizigo angani. Kuwasili Kwa ndege hiyo ni muendelezo wa uwekezaji wa Ethiopian Airlines katika kuongeza uwezo wa kuhudumia masoko ya kimataifa ya mizigo. Ujio wa ET-BAC unaongeza jumla ya ndege za mizigo za aina ya 777-200LRF ndani ya shirika hilo kufikia 12. Hatua hii inaimarisha uwezo wa shirika hilo kutoa huduma kwa masoko makuu duniani na kuendeleza nafasi yake kama kiongozi wa huduma za usafirishaji wa mizigo barani Afrika. #fleetexpansion #airline #ethiopianairlines✈️ #ethiopiancargo #aircargo #flywithethiopianairlines #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DKFGEgIMCDR/?igsh=Mmp1N2s4bGFheXVy *Ethiopian Airlines yapokea ndege mp...