Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 9, 2025 at 12:59 PM
https://www.instagram.com/reel/DKrjPckNXRJ/?igsh=MWU4M2x4Nm0zMTNqcg== *As Salaam Air yaongeza ndege ya nne aina ya Embraer 120.* Shirika la ndege la @assalaamairtz , lenye makao makuu visiwani Zanzibar, hivi karibuni limepokea ndege nyingine aina Embraer 120 yenye namba ya usajili 5H-LUF. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao wa Plane Spotter, ndege hiyo yenye iliwasili kwa mara ya kwanza katika Kisiwa cha Pemba juni 4 2025, ikitokea Zanzibar (ZNZ) na kutua salama katika Uwanja wa Ndege wa Pemba (PMA) majira ya saa 11:38 jioni Safari iliyochukua dakika 22 pekee. As Salaam ilianzishwa rasmi mwaka 2011 likifanya safari za Arusha-Zanzibar, Dar es Salaam-Pemba, Dar es Salaam-Zanzibar, Pemba-Dar es Salaam,Pemba-Zanzibar, Zanzibar-Arusha na Zanzibar-Pemba. Kwa sasa kampuni hiyo ina jumla ya ndege nne aina ya Embraer 120, kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 30. . #airline #assalaamair #fleetexpansion #newaircraft #assalaamair #embraer120 #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania

Comments