Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #flywithairtanzania
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Air Tanzania yafanya safari maalum kuwasafirisha mahujaji 105 kuelekea Hijja Shirika la Ndege la Air Tanzania @airtanzania_atcl limefanya safari maalum, kuwasafirisha mahujaji 105 kuelekea mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia, kwa ajili ya ibada ya Hijja ya mwaka huu. Kupitia taarifa rasmi, Air Tanzania imetoa shukrani za dhati kwa heshima waliyopewa na Baraza Kuu la Kiislamu kwa kulichagua shirika hilo kusafirisha mahujaji katika safari hiyo takatifu. Mwezi Machi mwaka huu, Shirika la Air Tanzania lilianza maandalizi ya kutumia ndege yake aina ya Boeing 737-9 kwa ajili ya kuwasafirisha waumini wa Kiislamu kwenda Saudi Arabia kwaajili ya ibada ya Hijja. Taarifa ya maandalizi hayo ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, machi 31 2025, alipohutubia Baraza la Eid lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kwa wakati huo, Air Tanzania ilikuwa kwenye hatua ya kuomba vibali kutoka katika mamlaka husika ili kuanza rasmi safari hizo. #airlines #airtanzania_atcl #flywithairtanzania #hijja #aviationlovers #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviata"
https://www.instagram.com/p/DKSExbgMLMw/?igsh=MWlya2xmczg5cGVzYQ== *Air Tanzania yafanya safari maa...