Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 30, 2025 at 03:17 PM
https://www.instagram.com/p/DKSExbgMLMw/?igsh=MWlya2xmczg5cGVzYQ== *Air Tanzania yafanya safari maalum kuwasafirisha mahujaji 105 kuelekea Hijja* Shirika la Ndege la Air Tanzania @airtanzania_atcl limefanya safari maalum, kuwasafirisha mahujaji 105 kuelekea mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia, kwa ajili ya ibada ya Hijja ya mwaka huu. Kupitia taarifa rasmi, Air Tanzania imetoa shukrani za dhati kwa heshima waliyopewa na Baraza Kuu la Kiislamu kwa kulichagua shirika hilo kusafirisha mahujaji katika safari hiyo takatifu. Mwezi Machi mwaka huu, Shirika la Air Tanzania lilianza maandalizi ya kutumia ndege yake aina ya Boeing 737-9 kwa ajili ya kuwasafirisha waumini wa Kiislamu kwenda Saudi Arabia kwaajili ya ibada ya Hijja. Taarifa ya maandalizi hayo ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, machi 31 2025, alipohutubia Baraza la Eid lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kwa wakati huo, Air Tanzania ilikuwa kwenye hatua ya kuomba vibali kutoka katika mamlaka husika ili kuanza rasmi safari hizo. #airlines #airtanzania_atcl #flywithairtanzania #hijja #aviationlovers #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviata

Comments