Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #indigoairlines
Posts
بھارت کی بدقسمت فلائٹ جو احمدآباد سے لندن تک پرواز...
بھارت کی بدقسمت فلائٹ جو احمدآباد سے لندن تک پرواز نہیں کرسکی، صرف احمدآباد ائرپورٹ کے ٹیک آف پوائنٹ...
Aviation Tanzania on Instagram: "Marubani wawili wa IndiGo wasimamishwa kazi baada ya ndege Yao kupatwa na dhoruba kali safarini. Mamlaka ya usafiri wa anga nchini India, imewasimamisha kazi marubani wawili waliokuwa wakirusha ndege ya IndiGo sina ya Airbus A321 Neo, baada ya kukumbwa na dhoruba kali ya mvua ya mawe angani, hali iliyosababisha taharuki kubwa na kuhatarisha maisha ya watu 227 waliokuwa ndani yake. Taarifa ya Mamlaka hiyo imeeleza kuwa ndege hiyo ilikumbwa na changamoto kubwa wakati ikielekea Srinagar, ambapo kwa kipindi fulani ilishuka kwa kasi ya futi 8,500 kwa dakika moja, kasi inayozidi mara nne kiwango cha kawaida cha kushuka. Wakati huo, mifumo kadhaa ya udhibiti wa ndege ilishindwa kufanya kazi, huku marubani wakipokea onyo la ndege kupoteza nguvu ya kuinuka pamoja na ongezeko la kasi kupita kiwango, hali iliyoonyesha jinsi walivyopambana kuirejesha ndege katika hali ya kawaida. Tukio hilo lilitokea katika safari namba 6E-2142 ambayo ilianzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, Delhi saa 10:55 jioni hadi katika Uwanja wa Ndege wa Srinagar saa 12:25 jioni. Maelezo zaidi yamebainisha kuwa marubani walijaribu kuwasiliana na waongozaji wa ndege wa Pakistan baada ya wale wa India kuwataka wasibadili mwelekeo kuelekea magharibi kutokana na vikwazo vya anga vinavyoendelea kati ya mataifa hayo. Hata hivyo, licha ya kupewa njia za mawasiliano na ATC ya Lahore, ombi la kubadilisha mwelekeo lilikataliwa. Afisa mmoja wa Mamlaka ya India amesema kuwa tukio hilo linaendelea kuchunguzwa, na kwamba marubani wote wawili wamesimamishwa kazi kwa muda wa uchunguzi. Waziri wa uchukuzi wa anga wa India alieleza kuwa tukio hilo ni la kushtua na linahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina. #severehailstorm #indigoairlines✈️ #pilots #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/p/DKKNF1JsOlK/?igsh=b2syMGwzdXBycThv *Marubani wawili wa IndiGo wasimamis...