Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #unrulypassenger

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Polisi wamdhibiti mwanaume aliyekuwa akiwashambulia maafisa wa usalama katika uwanja wa ndege wa Miami. Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 28 kutoka Toronto, Kanada,amekamatwa na polisi baada ya kuanzisha vurugu na kuwashambulia maafisa wa usalama wa usafiri wa anga (TSA) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, tukio hilo lilitokea saa moja asubuhi katika eneo la ukaguzi wa usalama ambapo mwanaume huyo, aitwaye Cameron Dylan McDougall, alianza kwa kumshambulia abiria mwenzake, kabla ya kuhamia kwa maafisa wa TSA waliokuwa kazini. Video ya usalama inaonesha McDougall akijaribu kumpiga afisa mmoja wa TSA kwa ngumi, kisha kumshika mikono na kuendelea kujaribu kumpiga. Alipojikwaa na kuanguka, afisa mwingine wa TSA alimshika miguuni ili kumzuia. Wakati wakijaribu kumdhibiti, McDougall alimpiga afisa mmoja ngumi tatu usoni. Mashuhuda wa tukio hilo walimshikilia McDougall hadi maafisa wa usalama walipowasili na kumtia mbaroni. McDougall sasa anakabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo kumpiga afisa wa usalama na mtumishi wa serikali, kumpiga mtu mwenye umri wa miaka 65, na kosa la kushambulia mtu mwingine. #airport #tsa #miamiinternationalairport #unrulypassenger #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKPOrLwMUyj/?igsh=MTBvdmp2Z3F3aDE0cA== *Polisi wamdhibiti mwanaume a...

Aviation Tanzania on Instagram: "Ndege yatua kwa dharura baada ya abiria kujaribu kufungua mlango angani. Ndege ya Shirika la Ndege la All Nippon Airways (ANA) iliyokuwa ikisafiri kutoka Tokyo, Japani kuelekea Houston, Marekani, ililazimika kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seattle-Tacoma baada ya abiria mmoja kutaka kufungua mlango wa dharura wakati ndege ikiwa angani. Kwa mujibu wa msemaji wa Idara ya Polisi ya Seattle, Chris Guizlo, tukio hilo lilitokea katikati ya safari, na abiria huyo alidhibitiwa kwa haraka na wafanyakazi wa ndege kwa kushirikiana na wasafiri wengine. Ndege hiyo ilitua salama katika uwanja wa ndege wa Seattle-Tacoma majira ya saa 10:19 alfajiri kwa saa za eneo hilo. Polisi waliomkagua abiria huyo na kubaini alikuwa katika hali ya matatizo ya kiafya, na alikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi. Hadi sasa, haijafahamika kama atafunguliwa mashtaka yoyote. Wakati ndege ikiwa bado kwenye uwanja huo, abiria mwingine alionyesha tabia isiyofaa naye aliondolewa ndani ya ndege na polisi. Kwa mujibu wa tovuti ya FlightAware, ndege hiyo iliendelea na safari yake kuelekea Houston saa 1:00 asubuhi. Kupitia taarifa yao rasmi, shirika la ndege la ANA limeeleza kuwa usalama wa abiria ni kipaumbele chao kikuu, na kuwapongeza maafisa wa usalama kwa usaidizi wao mkubwa. #emergencylanding #anaairlines #unrulypassenger #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKGuxksswjm/?igsh=MTRtc2YydWp0dmwxbg== *Ndege yatua kwa dharura baad...