Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 26, 2025 at 05:41 AM
https://www.instagram.com/reel/DKGuxksswjm/?igsh=MTRtc2YydWp0dmwxbg== *Ndege yatua kwa dharura baada ya abiria kujaribu kufungua mlango angani.* Ndege ya Shirika la Ndege la All Nippon Airways (ANA) iliyokuwa ikisafiri kutoka Tokyo, Japani kuelekea Houston, Marekani, ililazimika kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seattle-Tacoma baada ya abiria mmoja kutaka kufungua mlango wa dharura wakati ndege ikiwa angani. Kwa mujibu wa msemaji wa Idara ya Polisi ya Seattle, Chris Guizlo, tukio hilo lilitokea katikati ya safari, na abiria huyo alidhibitiwa kwa haraka na wafanyakazi wa ndege kwa kushirikiana na wasafiri wengine. Ndege hiyo ilitua salama katika uwanja wa ndege wa Seattle-Tacoma majira ya saa 10:19 alfajiri kwa saa za eneo hilo. Polisi waliomkagua abiria huyo na kubaini alikuwa katika hali ya matatizo ya kiafya, na alikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi. Hadi sasa, haijafahamika kama atafunguliwa mashtaka yoyote. Wakati ndege ikiwa bado kwenye uwanja huo, abiria mwingine alionyesha tabia isiyofaa naye aliondolewa ndani ya ndege na polisi. Kwa mujibu wa tovuti ya FlightAware, ndege hiyo iliendelea na safari yake kuelekea Houston saa 1:00 asubuhi. Kupitia taarifa yao rasmi, shirika la ndege la ANA limeeleza kuwa usalama wa abiria ni kipaumbele chao kikuu, na kuwapongeza maafisa wa usalama kwa usaidizi wao mkubwa. #emergencylanding #anaairlines #unrulypassenger #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments