RFI Kiswahili
February 11, 2025 at 07:31 AM
Rais wa Marekani🇺🇸 Donald Trump ameonya kuwa mkataba wa usitishwaji vita kwenye ukanda wa Gaza, utavunjika iwapo wapiganaji wa Hamas, hawatowaachia huru mateka wote wanaoendelea kushikiliwa kufikia siku ya Jumamosi wiki hii.
Onyo hili la rais Trump limekuja, baada ya Hamas kutishia kuahirisha zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel🇮🇱, baada ya kuishtumu nchi hiyo kuendelea kuvunja mkataba huo wa usitishwaji vita.👆
👍
😂
😢
9