
RFI Kiswahili
367.5K subscribers
Verified ChannelAbout RFI Kiswahili
Karibu katika chaneli ya Radio France International, idhaa ya Kiswahili. Fuatilia habari zetu kutoka Kila pembe ya Dunia.
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Israel 🇮🇱 imechapisha kanda ya video inayosema inaonyesha vikosi vyake vya uokoaji vikiwa katika eneo la shambulio la kombora la Iran 🇮🇷 🎥Reuters

Vituo vya mafuta jijini #tehran vimeshuhudia foleni ndefu wakazi wakisubiri kujaza mafuta kwenye magari yao na pikipiki wakati huu mashambulio ya Israel yakiendelea kuripotiwa katika mji huo siku ya Jumapili ya tarehe 15 Juni. Iran 🇮🇷 na Israel 🇮🇱 zimekuwa zikibaliana kwa makombora tangu Israel ilipoanzisha mashambulio yake makubwa zaidi ya anga dhidi ya Iran mapema Ijumaa Juni 13. Wakaazi wa Tehran wamesema wameshuhudia uhaba wa mafuta katika vituo vya mafuta kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa na uhitaji wa bidhaa hiyo haswa wale wanaopanga kuondoka jijini. "Kwa hakika watu wana wasiwasi," mkaazi mmoja wa Tehran alisema, na kuongeza kwamba hakukuwa na maeneo ya watu kupata hifadhi ya muda ikiwa dharura itatokea. 🎥Reuters

Rais wa Marekani🇺🇸 Donald Trump alikataa mpango wa Israel 🇮🇱wa kuuawa kiongozi wa juu wa kiroho wa Iran🇮🇷 Ayatollah Ali Khamenei, kulingana na taarifa ya maofisa wawili kutoka serikali ya Marekani. Kulingana maofisa hao, Trump alimwambia Benjamin Netanyahu mpango wake wa kumuua Khamenei haukuwa mzuri licha ya Trump mwenyewe kutozungumzia suala hilo hadharani. Inaripotiwa kuwa mazungumzo kati ya wawili hao yalifanyika tangu Israel ilipoishambulia Iran siku ya Ijumaa.


Milipuko hii inaripotiwa muda mfupi kupita baada ya jeshi la Israel🇮🇱 kuonya kuhusu shambulio jipya kutoka nchini Iran🇮🇷 na kuwataka raia kusalia katika maeneo salama hadi pale ambapo watakapopewa taarifa zaidi. 📷Reuters


https://vm.tiktok.com/ZMSfKmUE1/ Majengo manne yameripotiwa kuporomoka katika eneo la Mathura, kaskazini mwa India, kufuatia hali ya mbaya ya hewa iliyoshuhudiwa mapema Jumapili asubuhi. Vikosi vya uokoaji kutoka Shirika la Taifa la Kukabiliana na Maafa (NDRF) na Kikosi cha Jimbo (SDRF), kwa kushirikiana na maafisa wa zimamoto, manispaa na utawala wa eneo, wanaendeleza juhudi za kuwaokoa watu waliokwama chini ya kifusi kama unavyoona kwenye video hii 📷Reuters

Wanajeshi wa Israel🇮🇱 wamewaua raia 59 wa Palestina🇵🇸, 17 kati yao wakiuuawa wakati wakijaribu kufikia vituo vya kutoa chakula cha msaada kutoka kwenye wakfu wa missada unaoongozwa na Marekani🇺🇸 na Israel. Mauaji haya yameripotiwa na wizara ya afya kwenye eneo husika.


https://www.youtube.com/live/TNGPrq_3NxA?si=ky5vbOslSzQmVnK-

https://www.youtube.com/live/nMO8bDqSjIA?si=LcsKd_DrxGeNDKJ4

Iran italipia 'gharama kubwa' kwa vifo vya raia: Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin #Netanyahu leo Jumapili amezuru eneo la makazi ya watu karibu na #telaviv lililoharibiwa na shambulio la kombora la #iran. Ziara yake imejiri wakati huu juhudi zikiendelea kuwatafuta watu waliofukiwa chini ya vifusi vya jengo la ghorofa lililoporomoka katika mji wa Bat Yam, kusini mwa Tel Aviv. 🎥Reuters