RFI Kiswahili
February 11, 2025 at 05:59 PM
Waziri Mkuu wa #israel Benjamin #netanyahu amesema mwafaka wa usitishaji wa mapigano huko #gaza utavunjika iwapo Hamas haitawaachilia mateka Jumamosi ya wiki hii.
Kauli yake imejiri baada ya wapiganaji wa Hamas kudai kwamba hawataachia huru mateka watatu wa 🇮🇱 kama ilivyotarajiwa kutokana na madai ya ukiukaji wa usitishaji mapigano wa Israel.
#netanyahu amekiri kuwa jeshi la Israel liko tayari kurejea kwenye mapigano makali hadi Hamas washindwe.
😢
🙏
👍
❤️
😂
24