RFI Kiswahili
February 12, 2025 at 06:02 AM
Afrika Kusini🇸🇸 imeanza kuimarisha uwepo wake wa kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo🇨🇩. Takriban siku kumi zilizopita, Pretoria ilituma vifaa vya kijeshi na wanajeshi, kati ya 400 na 8,000 kulingana na vyanzo, katika jiji la Lubumbashi.
Afrika Kusini ilipoteza wanajeshi wake 14 katika vita vya hivi karibuni mashariki mwa jamhuri ya kidemkorasia ya Congo kati ya jeshi la FARDC na washirika wake pamoja na waasi wa M23 wanaungwa mkono na Rwanda🇷🇼 waliofaulu kuudhibiti mji wa Goma.
Taarifa zinasema Afrika Kusini sasa imeaongeza wanajeshi wengine ndani ya Kikosi cha kulinda amani Monusco pamoja na SamiDRC kikosi cha SADC.
Ripoti : Ali Bilali👆
🙏
👍
❤️
😢
😮
12