RFI Kiswahili

RFI Kiswahili

367.5K subscribers

Verified Channel
RFI Kiswahili
RFI Kiswahili
February 12, 2025 at 06:29 AM
Waziri Mkuu wa Israel🇮🇱 Benjamin Netanyahu ameonya kuwa nchi yake itasitisha mkataba wa usitishwaji wa vita na kundi la Hamas, iwapo mateka wote wanaoendelea kushikiliwa hawatoachiliwa huru kufikia siku ya Jumamosi. Kauli hii ya kiongozi huyo wa Israeli, inakuja baada ya rais wa Marekani🇺🇸 Donald Trump kuanza kutoa onyo hilo wiki hii. Netanyahu amewaagiza wanajeshi wa Israeli kujiandaa kuendelea na vita kwenye ukanda wa Gaza. Kundi la Hamas limetangaza kuwa limeahirisha zoezi la kuwaachia mateka kwa madai kuwa Israeli imekiuka masharti ya mkataba huo.
👍 ❤️ 😂 5

Comments