
RFI Kiswahili
February 15, 2025 at 04:06 AM
Mzozo unaoongezeka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unatarajiwa kupewa nafasi kubwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika unaoanza Jumamosi, huku rais wa DRC akiwa hayupo baada ya waasi wanaotuhumiwa kuungwa mkono na #rwanda kuingia katika mji wa pili mkubwa katika ardhi yake.
AU yenye mataifa 55 linakutana katika mji mkuu wa #ethiopia Addis Ababa huku Afrika ikikabiliwa na migogoro mikali haswa nchini #drcongo na #sudan pamoja na hatua ya Rais wa Marekani Donald #trump kupunguza misaada ya maendeleo ambayo imeliathiri vibaya bara Afrika .
Viongozi wa Afrika wanawakilisha takriban watu bilioni 1.5 katika muungano wa AU unaokosolewa kwa muda mrefu kwa uzembe na kutoa kauli zisizo tekelezwa.
❤️
🙏
👍
😂
😢
12