Swahili Times
February 13, 2025 at 09:11 AM
Polisi katika mji wa Eldoret nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha Collins Cheruiyot, kijana mwenye umri wa miaka 24, aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kuvunja na kuingia katika baa ya mama yake na kuiba pombe, kufariki dunia kwa kujinyonga akiwa rumande.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Turbo, Patrick Wekesa, Cheruiyot aliamua kujitoa uhai baada ya juhudi zake za kumshawishi mama yake kufuta kesi dhidi yake kugonga mwamba.
😢
😂
👍
❤️
😮
🙏
36