Swahili Times

Swahili Times

780.0K subscribers

Verified Channel
Swahili Times
Swahili Times
February 13, 2025 at 12:27 PM
Aliyekuwa Gavana wa Kiambu nchini Kenya, Fredinand Waititu amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela au faini ya Ksh milioni 52.5 [TZS bilioni 1.05] baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya utoaji zabuni kinyume cha sheria ya shilingi milioni 588 iliyomkabili yeye, mkewe na wengine watano. Waititu amehukumiwa pamoja na mkewe, Susan Ndung’u ambaye amepewa kifungo cha mwaka mmoja au faini ya shilingi ksh 500,000 [TZS milioni 10]. Aidha, gavana huyo amezuiwa kugombea wadhifa wowote hususan wa kisiasa kwa muda wa miaka 7.
😂 👍 😮 🙏 😢 ❤️ 38

Comments