Swahili Times
February 13, 2025 at 02:09 PM
Jeshi la Polisi mkoani Njombe linamshikilia Vinord Ndondole (37) mkazi wa Matemela Mbarali, Mbeya kwa kosa la kupatikana na meno ya tembo manne akiwa ameyafunga ndani ya mfuko wa salfeti kwenye pikipiki yake, akiyasafirisha kama mzigo wa kawaida.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, imesema meno hayo yana thamani ya TZS milioni 197.28.
😮
😂
👍
😢
🙏
❤️
26