Swahili Times

Swahili Times

780.0K subscribers

Verified Channel
Swahili Times
Swahili Times
February 13, 2025 at 08:32 PM
Tanzania imeshinda nafasi mbili zilizokuwa zikigombewa katika uchaguzi wa Taasisi za Umoja wa Afrika ambazo ni nafasi ya Mjumbe wa Tume ya Umoja wa Afrika inayohusiana na sheria za kimataifa, iliyokuwa ikigombewa na Profesa Kennedy Gastorn na nafasi ya Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika dhidi ya rushwa iliyokuwa ikigombewa na Benjamin Kapera. Profesa Gaston ameshinda kura 45 kati ya kura 48, na Kapera ameshinda kura 33 kati ya kura 48 zilizopigwa katika kikao cha 46 cha Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika.
👍 ❤️ 🙏 😂 😮 31

Comments