JamiiForums

JamiiForums

716.2K subscribers

Verified Channel
JamiiForums
JamiiForums
February 12, 2025 at 06:50 PM
MOROGORO: Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu imeanza kusafisha maeneo ya Mto Ngerengere, Mazimbu Manispaa ya Morogoro ili kuweka mazingira safi, kuruhusu maji kupita kwa urahisi na kupunguza athari wakati wa mafuriko Afisa wa Maji Bonde la Wami Ruvu Kidakio cha Ngerengere, Mhandisi Nangu Makula amesema zoezi hilo litaenda umbali wa Mita 900 (Mazimbu hadi Kihonda) Ikumbukwe Desemba 8, 2024, Mdau wa JamiiForums.com alitoa wito kwa taka zitolewe katika mto huo kwa kuwa zimechangia maji kuingia mtaani, akatolea mfano wanaokuwa hatarini zaidi ni Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na wale wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mahlangu Soma https://jamii.app/MtoNgerengereUsafi
🙏 ❤️ 👍 😂 😢 18

Comments