
JamiiForums
712.6K subscribers
Verified ChannelAbout JamiiForums
Karibu katika Chaneli yetu rasmi ndani ya WhatsApp. Pata taarifa za uhakika, kwa wakati | Tanzania
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa taarifa ya wito wa kufanyika kwa Sala na mfungo wa kuombea Haki na Amani nchini Agosti 23, 2025 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo leo Juni 20, 2025, imesema kuwa kila Jimbo, Parokia, Jumuiya za Kitawa na Taasisi wataweka utaratibu utakaowawezesha kusali na kutubu kwa masaa 12 au 24 kulingana na uwezo wa Mazingira Soma https://jamii.app/SalaKatolikiTZ


DAR: Kupitia Ukurasa wa X wa Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa Chama cha ACT - Wazalendo, Shangwe Ayo, amesema Polisi wamefika katika Ofisi za Chama hicho na kumkamata Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa, Janeth Rithe, kwa agizo la Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO Soma https://jamii.app/PolisiACTWazalendoJaneth


Kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Truth Social, Rais wa Marekani, Donald Trump ameandika "Siku nyingi za mapumziko zisizo za kazi nchini Marekani zinatugharimu mabilioni kwa sababu biashara nyingi hufungwa. Wafanyakazi nao hawapendi hali hiyo." Trump ametoa kauli hiyo Juni 19, 2025, katika Sikukuu ya Kitaifa ya "Juneteenth" ambayo husherekewa Juni 19 kila Mwaka kwa ajili ya kuadhimisha kuachwa huru kwa Waamerika Weusi waliokuwa Watumwa Trump ameongeza "Kwa mwendo huu tutakuja kuwa na sikukuu kila siku ya kazi. Hali hii lazima ibadilike kama kweli tunataka kuifanya Marekani kuwa na Nguvu tena." Pia Rais huyo hakuhudhuria wala kushiriki katika shughuli yoyote ya kuadhimisha sikukuu hiyo Soma https://jamii.app/MapumzikoHugharimuMarekani


DODOMA: Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akizungumza Bungeni leo, Juni 20, 2025 amesema wanaoendela kutukana waachwe waendelee kutukana Soma https://jamii.app/ZunguWatukane