
JamiiForums
February 13, 2025 at 09:01 AM
Mdau wa JamiiForums.com anadai kuna changamoto wakati wa kuhuisha Leseni za Daladala zilizopewa vibali Mwaka 2023 katika 'ruti' ya Mbezi - Bagamoyo kwa maelezo kuwa wamepewa kimakosa
Anaeleza wamefanya kazi kwa takriban Miaka 2 halafu Mwaka wa tatu huu wanaambiwa wamepewa leseni kimakosa, anahoji Je, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inawatendea Haki wamiliki na Abiria wanaosafiri kupitia njia hiyo?
JamiiForums imewasiliana na Afisa Mfawidhi LATRA - Pwani, Aisha Kuwa kuhusu hoja hiyo, amesema “Kwa Mkoa wangu wa Pwani hilo jambo halijafika kwangu. Kwa kawaida wakikataliwa kupewa Leseni huwa kuna maelekezo wanapewa, nadhani hilo ngoja tulifuatilie kwa ukaribu kujua kinachoendelea.”
Soma https://jamii.app/LATRAMbeziBMoyo
👍
😂
❤️
🙏
6