
JamiiForums
February 13, 2025 at 12:22 PM
Akijibu hoja ya Mdau wa JamiiForums.com kuwa kuna kero kwa Abiria wanaopanda Daladala za Mbezi - Mlandizi kwamba muda wa Jioni zinakatisha ruti, Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Pwani, Aisha Kuwa amesema wanachukua hatua kudhibiti hilo
Aisha amesema “Tumekuwa tukiendelea na ukaguzi kuanzia Asubuhi hadi Jioni, hayo Magari ambayo Mdau ameyalalamikia sio Jioni tu hata Mchana au Asubuhi wapo wanaofanya hivyo."
Ameongeza “Pia, ruti zote kuanzia Mbezi kwenda Mlandizi, Mbezi – Kwala, Mbezi - Mzenga tumesitisha utoaji wa leseni mpya kwa kuwa inaonekana Gari ni nyingi tofauti na idadi ya Abiria ndio maana kuna muda wahusika wanasitisha ruti kwa kuwa wanaona hasara kwenda na Abiria wachache hadi mwisho."
Soma https://jamii.app/LATRAPwaniLeseni
👍
❤️
😢
4