JamiiForums

JamiiForums

712.6K subscribers

Verified Channel
JamiiForums
JamiiForums
February 13, 2025 at 05:18 PM
Akizungumza katika mjadala wa "Kuelekea Uchaguzi, Tunatofautishaje Zawadi na Rushwa?", Mwanasiasa (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amesema “Hakuna anayeweza kubisha kuwa kuna matumizi makubwa ya Fedha katika Chaguzi zetu kiasi kwamba ni jambo gumu kutofautisha Rushwa na Zawadi nyakati za Uchaguzi na hasa katika Mwaka wa Uchaguzi” Ameongeza kuwa “Hali ya Rushwa sio tu kwa Wanasiasa bali pia hata kwa Dola, ndio maana nyakati za Uchaguzi unaweza kukuta Viongozi wakubwa wakitoa ahadi ambazo zinaweza kutafsiriwa au kutumika kama sehemu ya ushawishi wa nguvu zao kuelekea kwa Dola” Amesema unaweza kukuta Mgombea ni Rais au Waziri anaweza kutumia nafasi yake wakati wa Kampeni za Uchaguzi kutoa maelekezo ya kimamlaka na hivyo kutumika kama sehemu ya ushawishi wakati ni jambo ambalo halitakiwi kufanyika hivyo
👍 ❤️ 😂 😢 🙏 6

Comments