
JamiiForums
February 16, 2025 at 12:25 PM
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuwasilisha hoja akilitaka Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) kuwasaidia Wahitimu kwa kuwapatia Leseni mapema akidai wanapitwa na fursa nyingi Mtaani, ufafanuzi umetolewa na Baraza
Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa #tnmc, Ezekiel Nyalusi akizungumza na JamiiForums, amesema “Muuguzi akifaulu, anatakiwa kula kiapo, akiapishwa ndio anakabidhiwa Leseni na Cheti, kuna takribani Wauguzi 3,500 waliofaulu, hadi kufikia Februari 14, 2025 kati yao takribani 2,000 walikuwa wameshahakikiwa."
Ameongeza: “Kinachofanyika kwa sasa ni maandalizi ya mahafali, hivyo Mwanafunzi hataweza kuona Leseni yake hadi ale kiapo siku ya mahafali, inawezekana hali ya kisoko kwa sasa inachangia wahitaji Leseni haraka. Wawe na Subira, wasubiri mahafali.”
Soma https://jamii.app/LeseniMapemaTNMC
🙏
👍
😢
4