Radio Maria Tanzania
February 9, 2025 at 05:28 PM
PADRE CHRISTANTUS- KILA MMOJA ANATAFUTA UTAKATIFU, AMEWATAKA WAKRISTO KUWA WATU WA MATUMAINI
Wito huo umetolewa leo Februari 9, 2025 na Padre Christantus Julius chiwili,
Paroko Msaidizi Parokia ya Mlingano, kwenye Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa Mungu kwa Daraja Takatifu ya Upadre katika Parokia ya Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe - Mkata, Jimbo Katoliki Tanga.
Padre Chiwili ambaye pia ni Mkufunzi wa chuo cha Makatekista Jimbo Katoliki Tanga, amesema kila mmoja anapaswa kuwa daraja na sababu ya mwingine kuvuka katika safari ya Matumaini na kuufikia utakatifu.
Aidha, amesema ili kila mtu afikie Utakatifu anapaswa kuwa mtu wa sala ili neema za Mungu ziambatane naye katika Safari yake.
Hata hivyo, amesema Utakatifu unaenda sambamba na unyenyekevu na katika kuomba ndipo unapata msaada kutoka kwa Mungu.
Kadhalika amesema, Utakatifu sio kwa Mapadre na Watawa tu, hata wao wanasafari ya kuutafuta na kuufikia utakatifu, hivyo kila mmoja anapaswa kuendelea kujinyenyekeza huku akijikita katika sala.
Padre Chiwili ni miongoni mwa Mapadre 8 ambao walipadrishwa hivi Karibu, katika Jimbo Katoliki Tanga na leo Februari 9, 2025 wamehitimisha Misa za Shukrani kwa Mapadre wote ambao walipadrisho Pamoja.
Na Tumaini Endrick Mmambale, Radio Tanzania Tanga
www.radiomaria.co.tz
#radiomariatz
#injilishakwaharaka
#mahujajikatikamatumaini
🙏
❤️
👍
😂
😮
🫂
72