
Radio Maria Tanzania
350.5K subscribers
Verified ChannelAbout Radio Maria Tanzania
Sauti ya kikristo Nyumbani Mwako
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

SHEREHE YA EKARISTI JUNI 22, 2025 - PADRE BONAVENTURE MARO C.PP.S leo ni Sherehe ya Mwili na Damu Takatifu sana ya Bwana wetu Yesu Kristo, sherehe ijulikanayo kama 'Sollemnitas Sanctissimi Corporis et Sanguinis Christi'. Liturujia ya Neno la Mungu katika Sherehe hii inatutafakarisha kuwa, “EKARISTI TAKATIFU NI ISHARA YA UPENDO NA UKARIMU WA KIMUNGU” Sherehe hii huadhimishwa Alhamisi baada ya Sherehe ya Utatu Mtakatifu, lakini kwa sababu za kichungaji, katika majimbo mbalimbali huadhimishwa Dominika baada ya Sherehe ya Utatu Mtakatifu. Mama Kanisa ameamua hivyo ili kuwapa Watoto wake nafasi ya kufurahia, kumsifu, kumwabudu na kumpa Mungu heshima ya pekee katika fumbo la Ekaristi Takatifu, kwa maandamano yanayofanyika baada ya Misa Takatifu ili kuliishi, kulitafakari, kulishuhudia na kuonesha umuhimu na uhitaji wa Fumbo hili Takatifu katika Maisha yetu ya kiroho. Katika Sherehe hii ya Ekaristi Takatifu, tunamshukuru Mungu ambaye kwa mapendo makubwa alimtoa kwetu mwanaye wa pekee Bwana wetu Yesu Kristo, akatwaa mwili na kukaa kati yetu, akashiriki ubinadamu wetu ili atushirikishe Umungu wake na bado amebaki nasi kwa daima katika maumbo ya mkate na divai. Tuombe neema ya kudumu katika ushirika na Kristo, kwa kumpokea daima kwa imani na katika hali ya neema katika Ekaristi Takatifu ili tuweze kunufaika na matunda yatokanayo na kule kupokea kwetu Fumbo hili Takatifu. CHIMBUKO LA SHEREHE YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTO. Sherehe ya Mwili na Damu Takatifu sana ya Bwana wetu Yesu Kristo ilianzishwa rasmi katika Kanisa, kutokana na uwepo na kusambaa kwa ibada mbalimbali kwa heshima ya Ekaristi Takatifu, uwepo halisi wa Mungu katika maumbo ya mkate na divai mapema katika karne ya 13AD. Kwa kusaidiwa na wanateolojia mbalimbali na viongozi wa Kanisa kwa wakati huo, Sherehe hii iliadhimishwa kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1246 katika Jimbo la Liége huko Ubelgiji ikijulikana kama 'Corpus Christi', yaani Sherehe ya Mwili wa Kristo. Mwaka 1264 Baba Mtakatifu Urbano IV aliidhinisha Sherehe hii iadhimishwe katika Kanisa kote ulimwenguni. Alimwomba Mtakatifu Tomasi wa Aquino kuandika nyimbo na machapisho mbalimbali ya kiliturjia kwa ajili ya sherehe hii kama vile Pange Lingua, Tantum Ergo na Adore te. Mwaka 1263, uliotokea muujiza wa Ekaristi Takatifu huko Bolsena Italia ambapo Hostia Takatifu ilivuja damu wakati wa Ibada ya Misa Takatifu wakati ambapo Padre aliyeadhimisha alikua na mashaka juu ya uwepo halisi wa Kristo katika maumbo ya mkate na divai. Muujiza huu ulipeleka kukua na kusambaa kwa haraka kwa ibada kwa Ekaristi Takatifu na kwa namna ya pekee Sherehe hii ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo. Baadaye Mababa wa Mtaguso wa Trento (1545-1563) walifundisha kuwa, “Tunapaswa kumpa heshima Bwana wetu Yesu katika Ekaristi Takatifu hadharani ili wale wanaotazama Imani ya Wakristo Wakatoliki waweze kuvutwa na Yesu Ekaristi Takatifu, na kuweza kuamini katika Umungu wa Bwana wetu Yesu Kristo aliye hai na mzima katika Fumbo Takatifu sana la Ekaristi Takatifu” Hii ilitokana na kuwepo kwa mafundisho mbalimbali ya uzushi juu ya Ekaristi Takatifu juu ya uwepo halisi wa Kristo (Real Präsenz) katika maumbo ya Mkate na divai, kuabudu Ekaristi Takatifu nje ya Ibada ya Misa Takatifu na maandamano ya Ekaristi Takatifu. Katika majiundo ya mtaguso wa pili wa Vatikano 1962-1965, Sherehe hii iliunganishwa na Sherehe ya Damu Takatifu ya Yesu ambayo huadhimishwa tarehe 1 Julai, ili kusisitiza teolojia ya Ekaristi Takatifu, yaani Mwili na Damu Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hivyo jina lilibadilika kutoka 'Corpus Christi' yaani Sherehe ya Mwili wa Kristo na kuitwa 'Sollemnitas Sanctissimi Corporis et Sanguinis Christi', yaani Sherehe ya Mwili na Damu Takatifu sana ya Bwana wetu Yesu Kristo na ndivyo inavyojulikana hata sasa. MSINGI KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU. Imani yetu katika uwepo halisi na kweli wa Kristo katika maumbo ya Mkate na Divai upo katika maandiko Matakatifu ambapo ni Kristo mwenyewe alitoka mwili wake kama Chakula na Damu yake kama kinywaji kwa ajili yetu na akawapa Mitume wake mamlaka ya kuadhimisha fumbo hilo Takatifu kwa ukumbusho wake mpaka atakaporudi tena (Mt 26:26-29; Mk 14:22-25; Lk 22:14-20; 1 Kor 11:23-26 na Injili ya Yohane sura ya 6). Ndilo Adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu tunaloadhimisha kila siku, ukumbusho wa sadaka ya Kristo pale msalabani. Nini kinatokea katika mageuzo wakati wa ibada ya misa Takatifu? Katika ibada ya Misa Takatifu, mkate hugeuzwa kuwa mwili wa Kristo na Divai kuwa Damu ya Kristo, mabadiliko yajulikanayo kama Transubstantiation. Ndugu wapendwa, mababa wa mtaguso wa Trento wanasema hivi, “Kwa sababu Kristo Mkombozi wetu ndiye alisema mwenyewe kwamba huu ndio mwili wangu, akautoa mwenyewe kwa namna ya mkate na damu kwa namna ya divai. Hivyo kwa kutakatifuza mkate na divai hutokea mabadiliko ya kiini chote cha mkate kuwa katika kiini cha mwili wa Kristo Bwana wetu na kiini chote cha divai kuwa katika kiini cha damu yake”. Uwepo huu halisi na kweli katika maumbo haya ya mkate na divai huanza katika mageuzo na hudumu muda wote maumbo haya yanapokuwapo. Hivyo, Kristo yupo mzima na mkamilifu katika kila mojawapo ya maumbo ya mkate na divai na ni mzima na mkamilifu katika kila sehemu yao. Kwa jinsi hii, kuimega Ekaristi Takatifu hakumgawanyi Kristo hata kidogo. Uwepo wa Yesu unabaki kwenye kila kipande kidogo kilichovunjika hata katika kila tone la damu yake, uwepo wa Yesu umo kamili kabisa kama katika Ekaristi Takatifu nzima (KKK 1376-1377). Inaendeleaaaaaa.... Tunakutakia Tafakari njema mpendwa. #RadiomariaTanzania #Mahujajikatikamatumaini #Mariathon2025mamawamatumaini


NOVENA YA WATAKATIFU PETRO NA PAULO SIKU YA TATU NIA Ombea Wakristo wote wawe na umoja pasipo na utengano kuhusu kabila au hadhi zao. TAFAKARI wagalatia2: 7 “Lakini kinyume chake, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa Injili ya wasiotahiriwa kama vile Injili ya waliotahiriwa ilivyokuwa kwa Petro Tafakari: Kutobagua kwa Mungu: Kifungu hiki kinapinga wazo kwamba watu au vikundi fulani vinashikilia nafasi ya upendeleo machoni pa Mungu. Kukubalika kwa Mungu kunatokana na Imani si kwa hali au asili. Umoja wa Injili Licha ya maeneo tofauti ya huduma (Petro kwa Wayahudi, Paulo kwa Mataifa), Mitume walitambua injili sawa ya neema kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Usahihi wa ujumbe wa Paulo Uthibitisho wa Mitume juu ya huduma ya Paulo kwa Mataifa ulithibitisha ujumbe wake na kusisitiza kwamba wokovu unapatikana kwa wote wanaoamini sio tu wale wanaoshika sheria za Kiyahudi. Athari kwa leo Kifungu hiki kinatukumbusha kwamba msimamo wetu mbele za Mungu unaamuliwa na imani yetu katika Kristo si kwa makabila yetu msimamo wetu wa kijamii au malezi yetu ya kidini. Pia inahimiza umoja na ushirikiano miongoni mwa waumini kutoka asili mbalimbali kwa kutambua injili moja inayowaunganisha. Umuhimu wa neema Mistari hiyo inasisitiza kwamba wokovu ni zawadi ya neema ya Mungu si kitu kinachopatikana kupitia juhudi za kibinadamu au kushika sheria. Neema hii imeenea kwa wote wanaomwamini Yesu Kristo. Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Kitendo cha majuto Mungu wangu, najuta dhambi zangu kwa moyo wangu wote. Kwa kuchagua kutenda mabaya na kushindwa kutenda mema nimekutenda dhambi wewe ambaye nilipaswa kukupenda kuliko vitu vyote. Ninakusudia kwa msaada wako kufanya toba kutotenda dhambi tena na kuepuka chochote kinachoniongoza kwenye dhambi. Mwokozi wetu Yesu Kristo aliteseka na kufa kwa ajili yetu. Kwa jina lake Mungu wangu unirehemu. Amina Njoo Roho Mtakatifu Njoo Roho Mtakatifu, ujaze mioyo ya waaminifu wako na uwashe moto wa upendo wako ndani yao. Mpeleke Roho wako nao wataumbwa nawe utaufanya upya uso wa dunia. Ee Mungu, ambaye kwa nuru ya Roho Mtakatifu uliifundisha mioyo ya waaminifu utujalie kwa Roho Mtakatifu huyo huyo tuwe na hekima ya kweli na kufurahia daima faraja zake kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina. Maombi ya kufungua Baba wa Mbinguni, tunapokusanyika kuanza siku hii ya Novena kwa Watakatifu Petro na Paulo, tunaomba neema na mwongozo wako. Kupitia maombezi ya Mitume hawa Watakatifu tuimarishe Imani yetu na ututie moyo kufuata mfano wao. Fungua mioyo yetu kwa mapenzi Yako na ubariki nia zetu. Amina. MTAKATIFU PETRO NA PAULO NOVENA Baba wa Mbinguni, tunakuja mbele zako kwa mioyo minyenyekevu, tukitafuta maombezi ya Mitume wako waliobarikiwa Watakatifu Petro na Paulo. Nguzo hizi mbili za Kanisa letu, kupitia imani na dhabihu zao zimetuonyesha njia ya ufuasi wa kweli. Tunaomba mwongozo na Sala zao tunapojitahidi kumfuata Kristo kwa ukaribu zaidi kila siku. Mtakatifu Petro, ulichaguliwa na Yesu kuwa mwamba ambao Kanisa lake lilijengwa juu yake. Tusaidie kuwa na imani thabiti kama hiyo uliyoonyesha, hasa nyakati za majaribu na kutokuwa na uhakika. Utuombee ili tubaki waaminifu kwa wito wetu kama wafuasi wa Kristo na kuwa hodari katika Imani yetu. Mtakatifu Paulo, uliongoka kwa neema ya Mungu na ukawa mmisionari asiyechoka, ukieneza Injili hata miisho ya dunia. Tutie moyo kwa bidii yako kwa Imani na kujitolea kwako bila kuyumbayumba kwa utume wa Mungu. Utuombee ili tuwe na ujasiri wa kutangaza Injili kwa maneno na matendo yetu na kuwaleta wengine kwa upendo wa Kristo. Kwa pamoja Watakatifu Petro na Paulo, tunaomba maombezi yenu yenye nguvu kwa nia zetu maalum: (Taja nia yako hapa) Maombi yetu yainuliwe kwa utetezi wako mtakatifu na yawe yenye kumpendeza Mola wetu. Bwana Mungu, utujalie neema ya kuiga wema wa Watakatifu Petro na Paulo na kufaidika na mfano wao wa ufuasi wa kweli. Kupitia maombi yao na tuweze kukua katika Imani, tumaini, na upendo na siku moja tujiunge nao katika furaha ya milele ya Ufalme Wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina. Maombi ya Waongofu kwenye Imani Baba wa Mbinguni, Tunawaombea wale wote ambao ni wapya kwa Imani. Kwa msukumo wa mfano wa Mtakatifu Paulo na kukaribishwa kwake katika jumuiya ya Kikristo, naomba tuwakumbatie na kuwaunga mkono waongofu kwa mikono na mioyo miwili. Wape nguvu na faraja wanayohitaji wanapoanza safari yao katika Kristo. Tusaidie kuwa chanzo cha mwongozo na upendo, tukikuza mazingira ya kukuza ambapo waumini wapya wanaweza kukua katika imani yao na kupata nafasi yao ndani ya jumuiya. Matendo yetu na yaakisi upendo na kukubalika kwako tukisaidia kuyaunganisha kikamilifu katika Mwili wa Kristo. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina. Utukufu uwe kwa Baba, na kwa Mwana, na kwa Roho Mtakatifu. Kama ilivyokuwa hapo mwanzo na sasa na hata milele ulimwengu usio na mwisho. Amina. Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. www.radiomaria.co.tz #Salanisilaha #Mariathon2025 #RadiomariaTz


https://youtu.be/ItlWDGFsVtc?si=7EXBdT85BP2RY-bc

Tazama wanandoa wenye miaka 50, ambapo Juni 20, 2025 waliadhimisha Jubilei ya Dhahabu, ya Ndoa Takatifu ya Bwana Alex Mutagombwa na Bi. Georgia Kokulamuka, Wazazi wa Padre Almachius Mwemezi wa Jimbo Katoliki Rulenge Ngara. . . Picha na Goreth Lwamuzigu - Bukoba www.radiombiu.co.tz #RadiomariaTanzania #Mahujajikatikamatumaini #Mariathon2025mamawamatumaini


JUBILEI YA MIAKA 50 YA NDOA BWANA NA BI. ALEX MUTAGOMBWA, RUTABO - BUKOBA Picha wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Dhahabu, miaka 50 ya Ndoa Takatifu ya Bwana Alex Mutagombwa na Bi. Georgia Kokulamuka, Wazazi wa Padre Almachius Mwemezi wa Jimbo Katoliki Rulenge Ngara. Misa Takatifu iliadhimishwa nyumbani kwao, Parokia ya Mtakatifu Joseph - Rutabo, Jimbo Katoliki Bukoba na Padre Almachius Mwemezi wa Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, Homilia ilitolewa na Padre Godwin Rugambwa, Paroko wa Parokia ya Rutabo. . . Picha na Goreth Lwamuzigu- Bukoba www.radiombiu.co.tz #RadioMariaTz #Mahujajikatikamatumaini #Mariathon2025mamawamatumaini


LEO TUMEANZA WIKI YA 8 YA KAMPENI YA MARIATHON 2025, JE UPO NGAZI YA NGAPI? ▪︎ Karibu Sana Mpendwa Mtoto wa Mama tuendelee kukimbia kwa pamoja, Tupande NGAZI, Tuendelee kuweke alama ndani ya Utume wa Mama na Habari njema iwafikie watu wote. ▪︎ Makutano yetu ni 100200 (Namba ya Kampuni) Mpesa, Mix by Yas, Airtel Money na Halopesa. Pia kwa njia ya Benki CRDB 0150303128000 na Mkombozi Benki 00811515058001 karibi sana. 💃🏾💃🏾💃🏾 Mkono utoao, ndio upokeao... 🔥🔥🔥 Asante sana na Mungu akubariki na kukuongezea utakapo punguza. Amina. . . www.radiomaria.co.tz #RadioMariaTz #Mahujajikatikamatumaini #MamawaMatumaini


LEO TUMEANZA WIKI YA 8 YA KAMPENI YA MARIATHON 2025, JE UPO NGAZI YA NGAPI? ▪︎ Karibu Sana Mpendwa Mtoto wa Mama tuendelee kukimbia kwa pamoja, Tupande NGAZI, Tuendelee kuweke alama ndani ya Utume wa Mama na Habari njema iwafikie watu wote. ▪︎ Makutano yetu ni 100200 (Namba ya Kampuni) Mpesa, Mix by Yas, Airtel Money na Halopesa. Pia kwa njia ya Benki CRDB 0150303128000 na Mkombozi Benki 00811515058001 karibi sana. 💃🏾💃🏾💃🏾 Mkono utoao, ndio upokeao... 🔥🔥🔥 Asante sana na Mungu akubariki na kukuongezea utakapo punguza. Amina. . . www.radiomaria.co.tz #RadioMariaTz #Mahujajikatikamatumaini #MamawaMatumaini


LEO TUMEANZA WIKI YA 8 YA KAMPENI YA MARIATHON 2025, JE UPO NGAZI YA NGAPI? ▪︎ Karibu Sana Mpendwa Mtoto wa Mama tuendelee kukimbia kwa pamoja, Tupande NGAZI, Tuendelee kuweke alama ndani ya Utume wa Mama na Habari njema iwafikie watu wote. ▪︎ Makutano yetu ni 100200 (Namba ya Kampuni) Mpesa, Mix by Yas, Airtel Money na Halopesa. Pia kwa njia ya Benki CRDB 0150303128000 na Mkombozi Benki 00811515058001 karibi sana. 💃🏾💃🏾💃🏾 Mkono utoao, ndio upokeao... 🔥🔥🔥 Asante sana na Mungu akubariki na kukuongezea utakapo punguza. Amina. . . www.radiomaria.co.tz #RadioMariaTz #Mahujajikatikamatumaini #MamawaMatumaini
