Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
February 10, 2025 at 03:03 AM
WAZAZI WAFUNDISHENI WATOTO MAADILI, WATOTO WAONYWA KUTUMIA MIDOMO YAO VIBAYA Wito huu umetolewa jana Februari 9, 2025 na Padre Sylvester Msemwa wa Shirika la Karmeli (OCD)ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter Clavery Mbezi Louis, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu, ambapo amesema kama kuna kiungo kinachopaswa kusulubishwa ni Mdomo. Amesema Watoto wanapaswa kutumia vizuri Midomo yao na iwe na kazi ya kupeleka habari njema yenye kuleta Amani, Furaha na Matumaini kwa Wenzao ili kupitia udogo wao, Kanisa na jamii ipate watu bora na sahihi kwa kizazi cha sasa na baadae. Aidha Padre Silvester, amewataka watoto wote, kila mmoja atumie mdomo yake kuwasiliana vizuri na jamii ili wakue kiimani, kimwili na kiroho katika mazingira mbalimbali ambapo huleta mahusiano mazuri. Padre Msemwa ambaye ni Dekano wa Dekania ya Mtakatifu Augustino Mbezi louis, amewataka Watoto hao, wawe na midomo misafi kwa kusali kila wakati bila kuchoka na kushika Amri za Mungu na Kanisa, kwani kwa kufanya hivyo wataishi maisha ya Kumpendeza Mungu, Kanisa na jamii kwa ujumla. Akiendelea na Mafundisho yake Amesema kuwa, katika Mwaka huu wa Jubilei ya Ukristo 2025, Watoto watumie Midomo yao kupeleka Matumaini kwa Watoto wengine, hasa wanaoishi katika Mazingira Magumu kwa kuimba nao na kucheza pamoja kama Watoto Wakristo. Vile vile amewataka Watoto watumie Midomo yao kwa kusoma Neno la Mungu, kwani ni Taa ya Njia zao pia wasome Mafundisho ya Kanisa Katoliki ili wapate mwongozo wa maisha ya kiroho katika nyakati mbalimbali za Miasha. Padre Sylvester amehitimisha kwa kusema kwamba Wazazi wawarithishe na kuwafundisha Watoto vipaji vyao ili kuwakuza na kuwalea Watoto ndani ya Maadili ya Kanisa Katoliki, pia wamtumikie Mungu kizazi hadi kizazi kwani hayo ndio Malezi ya mtoto. Na Rosemary Kimario Radio Maria Tanzania- Dar es Salaam www.radiomaria.co.tz #injilishakwaharaka #mahujajikatikamatumaini #radiomariatz
🙏 ❤️ 👍 😢 😂 57

Comments