Radio Maria Tanzania
February 10, 2025 at 06:06 AM
ASKOFU MUSOMBA AWATAKA WAKRISTO WATATHIMINI NA KUTAFAKARI MAISHA YAO YA SAKRAMENTI
Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es salaam, Mhashamu Stephano Lameck Musomba OSA, amewataka Wanandoa kila wakati wanapo Adhimisha Jubilei ya ndoa zao wawe watu wa kutafakari hali na mwenendo wa Maisha yao ya ndoa na sio vinginevyo.
Wito huo ameutoa wakati wa Homilia yake katika Adhimisho ya Misa Takatifu ya Jubilei ya miaka 25 ya ndoa Tatatifu kutoka Parokia ya Mtakakatifu Kizito, Jimbo kuu la Dar es salaam.
Amesema Jubilei iwe chachu ya kufanya tathimini ya hali yao ya ndoa na iwasaidie kuongeza Upendo ndani ya familia na kumtukuza Mungu daima.
Kadhalika amewakumbusha Wanandoa kuwa watu wa sala za pamoja na kutambua ukuu wa Misa Takatifu ndani yao, kwani hizo ndizo silaa za kudumu katika Ndoa na sio vinginevyo.
Aidha Askofu Msaidizi Musomba amehitimisha Homilia yake huku aki wapongeza Wanandoa kwa kutimiza miaka 25 Jubilei ya ndoa huku akiwasihi, daima wadumu katika kusoma maandiko Matakatifu na kutafakari na Familia zao ili waweze kukua kiroho na kimwili.
Na Dominic Haule, Radio Maria Tanzania- Dar es Salaam
🙏
❤️
👍
😂
👏
😢
78