
Radio Maria Tanzania
February 10, 2025 at 12:25 PM
TUHITIMISHE NOVENA YA BIKIRA MARIA WA LURDI KWA SALA YA KUMWOMBEA MGONJWA
Ee Bwana Yesu Kristo ulishiriki ubinadamu wetu kwa hiari yako upate kuwaponya Wagonjwa na kuwaokoa Wanadamu wote.
Sikiliza kwa huruma sala zetu umjalie Afya ya Mwili na roho huyu ndugu yako.
Mfariji kwa kinga yako, mpe nafuu kwa nguvu yako.
Msaidie atumaini kupata wokovu kwa njia ya Mateso, kama ulivyotufundisha kutumaini hapo ulipoteswa kwa ajili yetu.
Utujalie sisi sote amani na furaha zote za Ufalme wako huko unakoishi milele na milele.
Amina.
#radiomariatanzania
#injilishakwaharaka
#mahujajikatikamatumaini
🙏
❤️
🤲
👍
😮
85