Radio Maria Tanzania
                                
                                    
                                        
                                    
                                
                            
                            
                    
                                
                                
                                February 10, 2025 at 07:59 PM
                               
                            
                        
                            NOVENA YA BIKIRA MARIA MFUNGUA MAFUNDO
SIKU YA TATU, JUMATATU FEBRUARI 10, 2025
Sala za utangulizi:-
👉🏽Nasadiki
👉🏽Sala ya Imani
👉🏽Sala ya matumaini
👉🏽Sala ya Mapendo
👉🏽 Sala ya kutubu
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
*Sala kwa Maria mfungua mafundo*
Mama yetu mpole Maria mfungua mafundo, chanzo cha amani na Furaha, unayajua maisha yangu vizuri kwamba yamejaa mafundo ambayo yananifanya nikose hewa mara kwa mara. Yamenifanya mfungua na hivi ninaomba ukombozi kutoka kwako mama.
Ninaaminia upendo wako wa kimama na ninajua kwamba kwa njia ya maombezi yako kwa mwanao, utayafungua moja baada ya jingine. Nataka kuishi maisha mapya ya mtoto wa Mungu a ninaamini kwamba bwana hataniacha bali atanipa maisha mapya ya mwili, akili na roho.
Naomba nisiwe peke yangu katika vita hivi vya rohoni, bali unielekeze na uniongoze ktk bonde hili la machozi.
Pamoja nawe kama msafiri mwandamana ninauhakika wa kuwa kwenye njia sahihi. 
Fungua Mafundo yangu yote leo ninaposubiri muda ule ambamo utafungua fundo la mwisho la maisha yangu nitakapokuwa huru mbali na dhambi zote na ninapomwona Bwana wetu uso kwa uso katika heri ya milele Mbinguni
 Amina 
🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Sali mafungu matatu ya Rozari
(Mafungu ya siku husika)
 Jumatatu
 
MATENDO YA FURAHA..
Somo la Biblia👇
Ikawa baada ya siku tatu, walimkuta hekaluni, ameketi Kati ya walimu akiwasikiliza na kuwauliza maswali; nao wote waliomsikia walimu akiwasikiliza na kuwauliza maswali nao wote waliomsikia walistaajabia ufahamu wake na majibu yake. Walipomwona walishangaa,na mama yake akamwambia, Mwanangu, kwanini umetufanyia hivi?Tazama, baba yako na mimi tumekutafuta kwa huzuni." Naye akawaambia"kwanini kunitafuta?Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya baba yangu?"Lakini hawakuelewa neno alilowaambia.Akashuka pamoja nao, akafika Nazareth,na aliwatii; Mama yake akayatunza maneno hayo yote moyoni mwake (Lk 2:46-51)
Ee Maria, wewe ni kielelezo chetu Cha tafakari Katika yote uliyopokea juu ya Yesu, hukuhoji Wala kutaka ufafanuzi lakini ulijifunza kuyaweka yote moyoni mwako. Chumba kilichofichika kinachofaa kwa tafakari na hakuna anayekijua au kukiona ila Mungu. Hekima gani unayo,Ee Maria. Kila akuonaye hukupa moyo mtulivu, matamu, yenye huruma na wazi.
Mama wa hekima nisaidie kutafakari yote katika ukimya huku nikiongea na Bwana ninapokukabidhi yote yanayotokea katika maisha yangu, huku nikiyapokea Kama mapenzi ya Mungu.
Mikononi mwako naliweka fumbo hili......(taja fundo) lililofanya maisha yangu kuwa magumu na ya kuumiza kwa miaka mingi.Sikiliza Sala yangu Maria mama wa shauri jema
Maria mfungua mafundo niombee mimi ninayekukimbilia
(Sali mafungu mawili ya mwisho ya rozari)
 
 
Sali pia Sala ya mwisho kwenye
 Novena ya kwanza
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
✝✝✝✝
SALA YA MWISHO
Bikira Maria mfungua mafundo
Maria mama yetu mfungua mafundo   kumbuka kwamba haijasikika kamwe kuwa aliyekukimbilia akitaka umsaidie ulimwacha bila kusaidiwa. Nikichochewa na matumaini hayo na nikielemewa na dhambi zangu na mateso yangu ninakimbilia ulinzi wako kwa moyo wa majuto Ee mama. Mama wa Neno la Mungu usiakatae maombi yangu lakini unihurumie na usikilize Sala yangu.
Unafungua mafundo yote katika maisha yetu Ule mkanda mrefu wa mafundo unanyooshwa katika mikono yako ya kimama na ya Mapendo Sasa nakuja kwako Ee Bikira wa mabikira, ona mafundo mangapi yananiziba pumzi maisha yangu. Unao  mateso ya maisha tena na tena.
Unaona nilivyopooza.Ee Maria uliyepata neema Imakulata mwenye kufungua mafundo katika maisha ya wanao naweka mikononi mwako marinda haya
👉🏽Changamoto za Kiroho
👉🏽Changamoto mahali ninapofanyia kazi
👉🏽Changamoto ninazozibeba katika maisha yangu na ambazo hazina ufumbuzi
👉🏽Mafundo yaliyosababishwa na tabia yangu, kukosa uvumilivu kukosa uwezo wa kuisikiliza, hasira, wivu, kutaka kulipa kisasi mashindano woga, chuki, kukosa usalama, kiburi, kutovutiwa na wenzake, hangaiko la moyo huzuni, urafi kushindwa, na uchoyo.
👉🏽Mafundo ya mioyo yetu iliyo migumu inayotuzuia kupenda kwa ukarimu na kusamehe kwa unahisi
👉🏽Mafundo yanayosabaishwa na matambiko,mazingaombwe, ushirika, uchawi, kupiga ramli.
👉🏽Mafundo kama matokeo ya kutoelewana katika familia Kati ya wazazi na watoto
👉🏽Mafundo ya kukosa ajira
👉🏽Mafundo ya msongo wa moyo kati ya mme na mke
👉🏽Mafundo yatokanayo na ulevi wa kupindukia na matumizi ya madawa ya kulevya
👉🏽Mafundo ya matokeo ya ugonjwa usiotibika
👉🏽Mafundo yanayosababishwa na maumivu Kutoka kwa wengine
👉🏽Mafundo yanayosababishwa na kuhukumiwa na dhamiri na utoaji wa Mimba.
Kwa unyenyekevu na kwa UTUKUFU wa Mungu tunakuomba ufungue mafundo haya yasiwepo tena milele. 
Tunakutumainia kwa kuwa wewe ni faraja yetu pekee Ee mama. Yapeleke yote kwa Yesu mwanao Bwana wetu.
Kwa maombezi yako yenye nguvu hakuna fundo hata moja linaloweza kubaki limefungwa.Kwa Imani kubwa tunatamani ulinzi wako wa pekee na wa uhakika maana hakuna aliyekimbilia msaada wako akakataliwa.
Maria mfungua mafundo utuombee kwa Mwanao na Bwana wetu sasa na hata milele.
Amina.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Amina
                        
                    
                    
                    
                    
                    
                                    
                                        
                                            🙏
                                        
                                    
                                        
                                            ❤️
                                        
                                    
                                        
                                            👍
                                        
                                    
                                        
                                            👏
                                        
                                    
                                        
                                            😘
                                        
                                    
                                        
                                            😭
                                        
                                    
                                        
                                            😮
                                        
                                    
                                    
                                        107